habari Mpya


Bashiru Ally -Awahimiza Wanakaragwe Kufanya Kazi kwa Bidii ili Kukuza Uchumi wao.

Bw.Bashiru Ally.

Na Elen Magambo –RK Karagwe 97.7

Wananchi wa Mkoa wa Kagera wametakiwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Ushauri huo umetolewa na Katibu Mkuu Taifa Chama Cha Mapinduzi Bw.Bashiru Ally wakati akisalimiana na wananchi wa wilaya ya Karagwe katika viwanja vya ofisi ya chama hicho mjini Kayanga.

Bw Ally amesema  uchumi wa mkoa wa kagera kwa asilimia kubwa unatengemea wananchi wa wilaya ya Karagwe,  Ngara na Kyerwa lakini bado baadhi ya watu wanaotumiwa na viongozi wa serikali kuwanyanyasa wananchi wanyonge kitendo amabcho hakikubaliki. 

SAUTI YA BW.BASHIRU AKIWA KARAGWE

Nao baadhi ya Wananchi wamesema wako tayari kutoa taarifa kwa Viongozi husika wanapoonewa kwani kwa sasa serikali inafanya kazi nzuri hasa kutatua changamoto zinazowakabili. 

Post a Comment

0 Comments