habari Mpya


Baba mzazi wa Anton Petro apangishiwa nyumba.

Ngara Kagera na Shaaban Ndyamukama.  
Baadhi ya wasamalia wema wamejitolea kumtafutia nyumba ya kupanga mzee Petro Magogwa wa kijiji cha Ngundusi wilayani Ngara baada ya matumaini ya kujengewa nyumba na millard Ayo kushindikana kukamilika kwa wakati
Mzee huyo ni yule aliyetishiwa kushtakiwa na mtoto wake Anthony Petro kituo cha Polisi Kabanga wilaya ya Ngara kwamba anataka kuuza shamba la familia kupata fedha za kutunza familia inayokabiliwa na changamoto za umaskini

Wasamaria hao wakiongozwa na Katibu wa kikundi cha Tumsaidie Anthony Petro kutoka ndani na nje ya wilaya ya Ngara Stella Rutaguza anayeishi mkoani Dodoma amesema nyumba iliyopatikana mzee huyo ataishi kwa muda  na watoto wake.  
Pamoja na hayo Afisa  ustawi wa jamii wilayani Ngara Mussa Balagondoza na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Aidan Bahama wamesema changamoto imekuwa ni upatikanaji wa fedha kutoa vyanzo vya mapato ya ndani. 
Viongozi hao wakati Anthony anaanza kutambulika kwenye mitandao ya kijamii kwa ujasili wa kumshtaki baba yake kumzuia  asiuze shamba, walimuahidi kununulia lingine  jipya na kunjengea nyumba kisha kumsomesha shule bora

Aidha ndoto za mtoto Anthony za kwenda likizo  wilayani Ngara kuonana na baba yake pia dada zake zimegonga mwamba, baada ya kukosekana fedha za kumtoa shule ya Amani Vumwe English Medium iliyoko Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Mfadhili wake anayemsomesha katika shule hiyo Isihaka Msuya amesema kwa sasa Anthony amempeleka nyumbani kwake hadi shule zitakapofunguliwa na kwamba katika mkataba wa kumsomesha Halmashauri ya Ngara ilitakiwa kumpeleka likizo na kumrudisha.
“Hapa nyumbani kwangu atapata huduma zote sawa na watoto wangu kinachotakiwa ni kumuendeleza apate elimu ya kuweza kumkomboa kwenye ndoto za maisha yake” Amesema Msuya.

Post a Comment

0 Comments