habari Mpya


14,046 Waliofaulu Waathirika na Ukosefu wa Miundombinu Kagera.

Wakati wazazi wa watahiniwa 25,499 waliofaulu mtihani wa darasa la saba mwaka 2018, wanajipanga kuwasajili watoto wao kidato cha kwanza mkoani Kagera, watahini 14,046 waliofaulu wanasubiri hatima ya ukamilikaji wa miundombinu mkoani humo.

Afisaelimu Mkoa wa Kagera Bw.Aloyse Kamamba, ametoa takwimu hizo wakati wa kikao cha kuwathibitisha wanafunzi watakaoingia mwaka 2019, kilichofanyika katika ukumbi wa Moorland Wilayani Ngara Disemba 14, 2018.

Kama mkoa tulipanga kiwango cha ufaulu cha 88%; jumla ya wanafunzi 25,499 wamepata nafasi za kujiunga na kidato cha kwanza 2019 kwa awamu ya kwanza kwa kuzingatia vyumba vya madarasa vilivyopo, miongoni mwao wavulana ni 14,356 na wasichana 13,143 sawa na 64.4%.” Alisema Bw.Kamamba.

Aidha, wanafunzi 14,046 wakiwemo wavulana 6,257 na wasichana 7,759 sawa na 35.52% wamefaulu, lakini kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa, wanasubiri ujenzi huo ukamilike, ili waweze kujiunga na shule za sekondari.

Wathiniwa waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2019 mkoani wa Kagera ni watoto 39,545, ambapo wavulana ni 18, 553 na wasichana ni 20,992, huku kiwango cha ufaulu mwaka 2018 kikipanda kwa asilimia 0.02% pekee.

Mwaka 2018 mkoa wa Kagera ulikuwa na watahiniwa 47,197, waliotarajiwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi, kati yao wavulana walikuwa 22,124, na wasichana ni 25,073, ambapo watahiniwa 86 walikuwa wenye mahitaji maalumu; wavulana ni 50, na wasichana 36.

Mchanganuo wa wanafunzi waliofaulu, lakini hawakupata nafasi kuoka kila Halmashauri mkoani Kagera ni kama ifuatavyo; wanafunzi 2160 kutoka Biharamulo, Bukoba DC 877, Bukoba Manispaa 1276, Karagwe 3086, Kyerwa 1876, Missenyi 578, Muleba 3696 na wanafunzi 256 kutoka Ngara.

Katika mwaka 2018 Mkoa wa Kagera umepata nafasi 143, kwa ajili ya shule za bweni, ufundi na ufaulu mzuri zaidi; na kati yao wasichana ni 49 ma wavulana ni 94, huku nafasi zikiongezeka 17 ilinganishwa na nafasi 126 ambazo mkoa ulipewa mwaka 2017.

Mgawanyo wa nafasi 23 za shule za sekondari za bweni kawaida kwa wasichana ni shule 04 alizozitaja kuwa ni Rugambwa, Tumaini, Kazima na Kigoma Bright, huku  wavulana wakiwa na nafasi 24 za bweni kawaida katika shule za sekondari 03 za Kigoma Bright, Moshi, na Shinyanga.

Wavulana 46 kutoka katika mkoa wa Kagera, watajiunga na shule za ufundi za Musoma na Bwiru, huku mgawanyo wa nafasi 05 za wasichana watakaojiunga na shule za ufundi kutoka mkoani humo.

Mkoa umepata nafasi za wanafunzi wenye ufaulu mzuri zaidi; wasichana wenye ufaulu mzuri zaidi wametengewa nafasi za bweni katika shule 02 za Msalato na Tabora wasichana; ambapo wavulana wametengewa nafasi katika shule 03 pia za Tabora wavulana na Mzumbe.

Mkoa umepata nafasi 94 za wanafunzi watakaojiuna na shule za bweni kawaida, ufundi na bweni kwa waliofanya vizuri zaidi kwa kila Halmashauri kama ifuatavyo; wavulana Biharamulo ni 09, Bukoba DC 12, Bukoba Manispaa 06, Karagwe 12, Kyerwa 12, Missenyi 08, Muleba 23, na Ngara 12.

Nafasi za wasichana kwa kila Halmashauri ni kama ifuatavyo; Biharamulo 03, Bukoba DC 09, Bukoba Manispaa 02, Karagwe 08, Kyerwa 06, Missenyi 02, Muleba 13, pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Ngara yenye nafasi 06, ambapo jumla ya nafasi 46 ni za wasichana pekee. 

Post a Comment

0 Comments