habari Mpya


Wasaidizi wa Kisheria mkoani Kigoma wapewa Mafunzo.

Na Adrian Eustace kutoka Kigoma.
Serikali kwa kushirikiana na wadau wa masuala ya kisheria nchini, wameanza kutoa mafunzo rejea kwa wasaidizi wa kisheria mkoani Kigoma ili kuimarisha utoaji wa huduma hizo na kuongeza ujuzi ufanisi katika utatuzi wa migogoro inayofanywa na wasaidizi wa kisheria.
 Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yanayoendelea mkoani Kigoma mratibu wa mradi wa utetezi wa haki za binadamu kutoka taasisi ya BAK-AIDS mkoani Kigoma BW.Juma Bewa amesema mafunzo yanayotolewa yamelenga kuwajengea uwezo zaidi wasaidizi wa kisheria.


Amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia wasaidizi wa Kisheria   kufanikisha majukumu yao pamoja na kuelewa Sheria mpya inayotambua kazi za msaada wa kisheria iliyopitishwa na bunge na kusainiwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dakt.John Pombe Magufuli.

Post a Comment

0 Comments