habari Mpya


Wananchi Ngara -Msitegemee Serikali kwa Kila Kitu,Tatueni Matatizo yenu Wenyewe.

Wananchi wilayani Ngara mkoani Kagera  wameshauriwa kujenga tabia ya kutatua matatizo yao wenyewe, badala ya kusubiri Serikali iwafanyie kila kitu, kwani vitu vingine viko ndani ya uwezo wao.

Hayo ameyasema November 16,2018 na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmahsauri ya Wilaya ya Ngara Bw. Aidan John Bahama wakati akikagua maadalizi ya kuwapokea watoto wa awali, wa darasa la kwanza na wa kidato cha kwanza Januari 2019.

Ziara hiyo iliwajumuhisha Mkuu wa Wilaya ya Ngara Lt. Col. Michael Mntenjele, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Bw. Aidan John Bahama, pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ngara Bw. Vedastus Tibaijuka.

“Tutapeleka fedha za miradi ya maendeleo kwa wananchi, ambao wamejidhatitti kutatua matatizo yao wenyewe, bila kusubiri serikali iwafanyie kila kitu.” Alisema Bw. Bahama.

Amesema ni ajabu kuona kwamba hata kuchimba choo, taasisi inategemea fedha ya Serikali, ambapo Wananchi wenye watoto katika taasisi husika wapo tu, huku akiagiza Wazazi kujitolea kuandaa vifaa kama vile mawe, tofali na mchanga na Halmashauri itasaidia vifaa vya viwandani.

Hata hivyo, imeonekana kuna haja ya wataalamu kutoka Halmashauri, kuwaelimisha wananchi  juu ya umuhimu wa kujitolea huku akiwaahidi, kuwasaidia gari la kusomba mawe, tofali na mchanga.

Wakati huo huo, Mkuu wa Wilaya ya Ngara Lt. Col. Michael Mntenjele, amewataka wananchi wote wilayani humo, kujenga vyumba vya madarasa vya kudumu kwa kutumia tofari za kuchoma, hata kama watachukua muda mrefu.

Amesema hayo baada ya kugundua kwamba wananchi, wanajenga vyumba vya madarasa kwa kutumia tofari mbichi, kwa madai kwamba wanafanya hivyo, ili kukidhi mahitaji wakati wanajipanga kujenga vyumba vya kudumu.

Amewahasa kwamba kufanya hivyo ni kufanya kazi mara mbili, na wanatumia gharama kubwa, kwani baada ya kujenga vyumba vya kudumu; vyumba hivyo havitatumika tena, na vitakuwa havina maana yoyote.

Post a Comment

0 Comments