Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli November 10,2018 amefanya
mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri kwa kuteua Mawaziri wawili na Naibu
Mawaziri wanne.
Kwanza, Rais Magufuli amemteua Japhet Ngailonga Hasunga kuwa Waziri wa
Kilimo.
Kabla ya uteuzi huo Hasunga alikuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, na
anachukua nafasi ya Dkt. Charles John Tizeba ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Pili, Rais Magufuli amemteua Joseph George Kakunda kuwa Waziri wa
Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Kabla ya uteuzi huo Kakunda alikuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), na anachukua nafasi ya Charles John
Mwijage ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Tatu, Rais Magufuli amemteua Constantine John Kanyasu kuwa Naibu Waziri
wa Maliasili na Utalii. Kanyasu anachukua nafasi ya Hasunga ambaye ameteuliwa
kuwa Waziri wa Kilimo.
Nne, Rais Magufuli amemteua Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa kuwa Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Kabla ya uteuzi huo Dkt. Mwanjelwa alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo.
Tano, Rais Magufuli amemteua Mwita Mwikwabe Waitara kuwa Naibu Waziri wa
TAMISEMI. Waitara anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Kakunda ambaye ameteuliwa
kuwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Sita, Rais Magufuli amemteua Mhe. Innocent Lugha Bashungwa kuwa Naibu
Waziri wa Kilimo. Bashungwa anachukua nafasi ya Mhe. Dkt. Mwanjelwa ambaye
ameteuliwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora.
Uteuzi wa viongozi hawa umeanza tarehe 10 Novemba, 2018 na wateule wote
wataapishwa Jumatatu tarehe 12 Novemba, 2018 saa 3:00 asubuhi, Ikulu Jijini Dar
es Salaam.
Wakati huo huo, Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya
Korosho Mama Anna Margareth Abdallah na kuivunja bodi hiyo kuanzia leo tarehe
10 Novemba, 2018.
|
0 Comments