habari Mpya


Msanii wa muziki wa Injili Geofrey Katilimbe aja na wimbo maalum kwa wanandoa.Pichani juu ni msanii chipukizi wa Muziki wa Injili Bw.Geofrey Katilimbe Mdodelo.
Msanii huyu wa Muziki wa Injili anaefahamika kwajina la Bw.Geofrey Katilimbe Mdodelo mkazi wa Wilayani Nngara mkoani Kagera ameachia wimbo wake mpya kwaajili ya wanandoa ambao ndoa zao zimefungwa Kanisani.


Wimbo huo unaenda kwa jina la “NIMEKUCHAGUA WEWE”  amesema kuwa ameutunga kwaajili ya wanandoa ambao ndoa zao zimehalalishwa na Mwenyezi Mungu.
 
“Nimetunga wimbo huu kwanza kuonesha uwepo mkubwa wa Mungu na pia mwanaume kuonesha thamani kubwa kwa Mwanamke na kuamini kuwa mke huyo mwema aliye mpata ni zawadi kutoka kwa Mungu”alisema Bw.Geofrey.

“Katika maisha ya mwanadamu mafanikio yote huja kutokana na Baraka kutoka kwa Mungu hivyo sifa,heshima na utukufu apewe Mungu kwakuwa kila ananye muomba Mungu kwa kuweka juhudi katika maombi yake siku zote hufanikiwa”aliongeza Bw.Geofrey.


Kwasasa msanii huyu ameachia Audio na kwamba video inaandaliwa hivyo mashabiki zake wajiandae kuipokea kazi hiyo ambapo Audio yake ameizindua rasimi octoba 27,2018 .

Geofrey  amesema kuwa anandoto zakufika mbali katika uinjilishaji kwanjia ya Nyimbo za dini hivyo anaomba Support kutoka kwa mashabiki zake ili kumuwezesha kufika mbali.   
Post a Comment

0 Comments