habari Mpya


Msako wa Nyavu za Uvuvi Haramu Chato, Wavuvi Waamua Kuziteketeza.

Baadhi ya Wavuvi wamebainisha kuwa uvuvi haramu umewaathiri hasa kwa kukosa samaki kwa wingi kwani Wavuvi haramu wanavua hadi mazalia hali inayosababisha samaki kupungua.

Na Elias Zephania RK Chato 97.7

Wakati Serikali wilayani Chato mkoani Geita ikiendelea na oparesheni za kutokomeza uvuvi usiofuata sheria ndani ya ziwa victoria, baadhi ya wavuvi wamejitokeza na kusema kuwa wamechoka kukimbizana na askari ziwani na hivyo wameamua kununua mafuta na kuteketeza vyavu zao kwa moto pasipo kusimamiwa na kiongozi yeyote.

Wakiongea na radio kwizera baada ya zoezi hilo, wameeleza kuwa walikuwa wakifanya kazi za uvuvi usiofuata utaratibu kutokana na umasikini na wameiomba serikali kuwaona kama walivyo wanyonge wengine hapa Nchini kwa kuwasidia zana za uvuvi wa kisasa ili wasikae bila shughuli ya kufanya.


BOFYA HAPA KUWASIKILIZA WAVUVI

Kwa upande wake mwenyekiti mwenye dhamana ya kuhifadhi rasilimali za uvuvi wilayani Chato Bw. Bashiri Manampha amesema kuwa ana wasiwasi huwenda wavuvi hao wakarudi kuharibu mazaria na makulio ya samaki endapo serikali haitachukua hatua za makusudi kwa kuwakopesha nyavu zinazokubalika kisheria na wakaendelea na shughuli hiyo.

Bw.Manampha amewataka wavuvi hao walioamua kuteketeza nyavu zao kwa hiari kuhakikisha wanabuni shughuli nyingine za kuwaingizia kipato kama vile kilimo cha bustani za mbogamboga na matunda, wakati wakisubiria ombi la kukopeshwa nyavu zinazokubalika kisheria.

Post a Comment

0 Comments