habari Mpya


Kaya Elfu 7 Zaondolewa TASAF wilayani Sengerema kwa Kukosa Sifa.

Busisi.

Na Erick Ezekiel –RK Sengerema 90.5/97.7  

Kaya elfu 7 zimeondolewa katika mfuko wa kunusuru kaya masikini   (TASAF) wilayani Sengerema mkoani Mwanza baada ya kukosa na sifa za kuendelea kunufaika na mpango huo.

Hayo yameelezwa na mkuu wa wilaya  ya Sengerema Bw. Emmanuel Kipole kufuatia baadhi ya wakazi wa kijiji cha Juma Kisiwani kulalamikia kitendo cha baadhi ya  kaya  zenye uwezo kuingizwa kwenye  mfuko  huo na kuwekwa pembeni kaya  zenye  maisha duni.


Bw.Kipole  amesema kuwa tangu  mwaka 2016  hadi Novemba  mwaka huu  kulikuwa na jumla ya kaya elfu 16 zilizokuwa zikinufaika na mpango huo    na kwamba kati ya kaya hizo,  kaya  7 zimeondolewa katika mpango huo kutokana na kutokuwa na sifa.

BOFYA KUMSIKILIZA DC KIPOLE 

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Juma-kisiwani wamemweleza kuwa ipo haja ya serikali kuangalia upya namna ya kutenda haki kwa walengwa wa mfuko huo ambao hawakupata nafasi.

Post a Comment

0 Comments