habari Mpya


Askofu Vithalis :Waamini fanyeni kazi kwabidii Ili kukuza Uchumi wa Taifa

BIHARAMULO NA SHAABAN NDYAMUKAMA, RK:

Waamini wa madhehebu mbalimbali  ya kidini wametakiwakufanya kazi kukuza uchumi na kuacha maisha tegemezi katika ngazi ya familia, na taifa kwa ujumla lakini wakijihadhari na matendo maovu yanayosababisha kuchuma dhambi  katika maisha ya duniani na kupata hukumu mbaya ya Mungu huko mbinguni.

 Hayo yametajwa na Askofu wa kanisa la Anglikan dayosisi ya Biharamulo Vithalis Yusuph katika ibada ya jumapili  ya majilio na kuwahimiza waumini hao kujiongezea mapato kwa kutumia majaliwa ya rasilimali ikiwemo mikono na akili katika mazingira yanayowazunguka.
Askofu Yusuph amesema muumini anatakiwa kuwa na maisha ya kiroho duniani kwa kuzalisha mali katika familia kisha kutoa sadaka ya kanisa na zaka katika kumshukuru mungu kwa maisha ya duniani na majaliwa ya mbinguni

Amesema umaarufu wa mwanadamu hata kama ni kutangaza kuokoka lazima ajivunie kuwa na uchumi ndani ya kaya yake kama chakula cha kutosha, mifugo, makazi bora kuwekeza katika elimu kwa watoto  kuwapa urithi wa maisha yao.
"Ukiwa na dhambi huwezi kuwa na akili ya kufanya biashara , mwaminifu katika ndoa na kuendelea maisha tegemezi na kufanya utapeli kwa wengine" Amesema Askofu Yusufu.

Amewashauri vijana kufanya kazi  halali za aina mbalimbali zinazopatikana kwenye mazingira yanayowazunguka kujipatia kipato kwa kujiajiri na kuacha kujiona wakivaa milegezo na kujilemba bila uchumi kwa kuwa maandiko yanasema asiyefanya kazi na asile.

Vile vile amewasihi kuacha mikono ya ubahiri lazima mapato yao wamtolee Mungu katika shughuli za kiroho na kijamii  lakini kulipa kodi kwa mamlaka iliyo juu yao  kuweza  ili kufanikiwa malengo ya duniani na mbinguni.

Katika hatua nyingine amewashauri watendaji wa umma na kanisa wakiwemo wawakilishi wa wananchi kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu kutimiza ahadi zao kwa kuwa chumvi ya duniani na nuru mbele za Mungu.

Katika ibada hiyo waamini wa kanisa la Anglican kata ya Kabanga wilayani Ngara ambao wanapatikana ndani ya dayosisi ya Kagera wanaounda kwaya ya Nuru wamechangia mifuko 15 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa kanisa kuu linalohitaji zaidi ya Sh800 milioni  katika dayosisi  mpya ya Biharamulo
Post a Comment

0 Comments