habari Mpya


Abiria na Magari yakwama Nyabugombe,Biharamulo kisa Magari mawili Kuharibikia Barabarani.

 Na Shaaban Ndyamukama, RK Biharamulo.

Magari ya mizigo na abiria zaidi ya 200 yanayosafiri kutoka na kwenda mikoa ya ndani na nje ya Tanzania yamekwama katika mlima wa Nyabugombe wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera baada ya magari mawili kiharibikia katika  eneo hilo na kusababisha mengine kushindwa kupita.

 Magari hayo yaliyokuwa na  mizigo ya aina tofauti tofauti yakitoka  bandari ya Dar es Salaam, Tanzania  kwenda Nchi za Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC  na mengine ya usafiri wa umma yaliyokuwa na abiria yalikwama eneo hilo kwa saa kadhaa.
Chanzo cha mkwamo huo ni magari mawili kushindwa kupanda mlima  huo wa wa Nyabugombe  kutokana na kuharibika baadhi ya Vipuli na inadaiwa yamekuwepo tangu Jana November 7,2018 majira ya jioni ambapo vipuli vinavyohitajika vimeagizwa hivyo haijulikani magari hayo yatatoka lini.

Katika eneo hilo pande zote za barabara zimezungukwa na makorongo kwenye safu za milima mpakani mwa wilaya ya Ngara na Biharamulo huku wasafiri wakikosa huduma muhimu za kijamii kama chakula, maji na mawasiliano kwa kuwa hakuna mtandao kuweza kupiga simu.
Akizungumza  na tovuti hii leo Novemba 8,2018,Mmoja wa abiria kutoka DRC MOKE KALUME amesema wasafiri wa magari ya mizigo na abiria wanateseka kwa kuwa magari hayatoki na wamekaa zaidi ya masaaa matano tangia asubuhi na kwamba yeye na wenzake walikuwa katika basi la Trinity kutoka Kigali kwenda jijini Dar es Salaam.

Naye dreva wa gari la abiria  aina ya Coasta la OBM linalotoka Kigali kwenda Kahama YUSPHORO MAKALA  ameshauri serikali ya Tanzania za nchi za Afrika mashariki na kati kuungana kutengeneza barabara ya kutoka Nyakanazi hadi Rusumo wilayani Ngara kwa kuwa inaingiza mapato mengine kiuchumi na bidhaa zinazopitishwa zinalipiwa kodi.
Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera SAADA MALUNDE ameahidi kuwasiliana na wakala wa barabara nchini TANRODS walioko ofisi za mkoa kuweza kufika na kubaini changamoto hivyo kisha kuitafutia ufumbuzi.

Amesema serikali iko katika mchakato wa kumpata mkandarasi wa kufanya marekebisho ya mashimo mengi ya barabara kwani inatambulika kuwa imetumika muda mrefu tangu kutengenezwa kwake na kwamba viongozi wa Nyabugombe waalikane kulinda abiria na Mali zao kuepuka uhalifu unaoweza kujitokeza.

Post a Comment

0 Comments