habari Mpya


Zimamoto Kagera yatoa Elimu ya Kukabili Majanga ya Moto kwa Watawa na Mapadre Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara.

Na-Shaaban Ndyamukama, RK Ngara.

Wamiliki wa Taasisi za dini, Mashirika ya umma pamoja na makampuni katika wilaya mbalimbali mkoani Kagera wametakiwa kuweka miundombinu ya  kujihadhali na majanga ya moto katika taasisi wanazosimamia kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza ya kuteketeza mali au kusababisha watu kupoteza maisha.

Wito huo umetolewa katika Semina ya kujihadhali na matukio ya moto kwa Watawa na Mapadre wa Jimbo katoliki la Rulenge Ngara  inayofanyika katika  parokia ya Buhororo wilayani Ngara

Akitoa mafunzo hayo hii leo October 17,2018  kwa wasimamizi wa imani za kiroho,  Afisa wa Zimamoto  wilayani Ngara,mkoani Kagera, Edward Bishangwa amesema matukio ya zimamoto yanasababisha kurudisha nyuma maendeleo kiuchumi na kukwamisha juhudi za kujinasua na changamoto za umaskini.
 Bishangwa amesema kuwa taasisi mbalimbali ikiwemo za kidini zinaanzisha miradi ya uwekezaji katika elimu kwa kuwa na shule za msingi na sekondari,zahanati na Hospitali hivyo kunatakiwa kuwa na vifaa vya zimamoto kwenye majengo  hayo ikiwemo  nyumba zao za kuishi  ili kukabili majanga ya moto unaoweza kujitokeza sambamba na kupata mafunzo ya kielimu  ya utambuzi wa matumizi ya vifaa hivyo.

Amesema katika ujenzi wa majengo lazima kutumia ramani zilizokaguliwa na idara ya zimamoto na kuelekezwa jinsi ya kuweka miundombinu ya vifaa vya kuzima moto kuepuka ajali  inayosababisha maafa au ulemavu wa kudumu

Amesema uanzishwaji wa miradi ya kiuchumi ni pamoja na uanzishwaji wa mashamba kwa kulipia kiasi cha fedha kama kodi ya serikali na kufanya miradi husika kwa uhuru zaidi lakini kupewa mbinu za kukabiliana na matukio ya ajali kwa kutoa taarifa katika mamlaka husika kupitia namba 114 ya idara ya zimamoto.
Hata hivyo Askofu wa jimbo katoliki la Rulenge Ngara Severine Niwemugizi amesema kanisa limelenga kutoa elimu ya zimamoto kwa mapadre na watawa kutokana na  na matukio ya ajali yanayotokea  ndani na  nje ya jimbo hasa wilayani Ngara na kusababisha madhara kitaifa. 
 

Naye  Afisa mwingine wa Idara ya Zimamoto Denis Minja ametoa wito kwa watumiaji wa vyombo vya moto kama magari na pikipiki wanatakiwa kuzingatia elimu na sheria zinazotaja kulinda usalama wao na kutoa taarifa kwa kupiga simu  namba 114 ya idara ya zimamoto.

Amezitaja njia za kusambaza moto kuwa ni mpitisho kwa njia za chuma, mnunurisho mfano moshi, miale au cheche kama   jua na kwamba visababishi vikubwa vya moto ni binadamu katika shughuli za maisha ya kila siku zikiwemo imani za kiushirikina

Post a Comment

0 Comments