habari Mpya


Wanafunzi wa Awali wanasomea Nje Kata ya Muganza wilayani Ngara.

Na Shaaban Ndyamukama, RK Ngara.

Wanafunzi 160 wa elimu ya awali  wenye umri wa miaka 9 hadi 11 wanasomea kwenye jengo la Kanisa la Asemblies Of God kutokana na ukosefu wa  vyumba vya madarasa katika kitongoji  Bitunga, kijiji cha Mukalinzi  Kata ya Muganza wilayani Ngara, mkoani Kagera.

 Baadhi ya wanafunzi wanazuiwa  kusomea shule  jirani ya Byamatongo iliyoko umbali wa kilomita nne kutoka kwenye kijiji hicho  kwenda  nchini Burundi ambapo wanazuiliwa kujifunza mitala na lugha ya nchi hiyo

Akizungumza jana mbele ya wanahabari waliotembelea wanafunzi hao , Mwalimu Elias Sprian anayejitolea kuwafundisha  alisema, kitongoji hicho kiko umbali wa kilomita kumi (10) hadi shule ya kijiji ya Rwimbogo ambapo wanafunzi wenye umri mdogo wanashindwa kutembea umbali huokwenda na kurudi kila siku.

Mwalimu huyo aliyehitimu kidato cha nne katika shule ya sekondari ya kata ya Muganza mwaka 2014, aliamua kufundisha watoto hao kujua kusoma kuhesabu na kuandika akilipwa na wazazi kiasi cha Sh40,000 kwa mwezi.
Alisema katika kitongoji hicho wanafunzi wanalilia kwenda kusomea nchi jirani ya Burundi lakini mitaala ya elimu ya nchi hiyo inatofautiana na  mfumo wa elimu wa Tanzania  kwani kule wanafundisha kwa lugha ya Kirundi na kifaransa.

“Wananchi wa kitongoji hiki wengi hawajui kusoma na kuandika na baadhi  ya wanafunzi wanaishia njiani kwa utoro, mimi   nilifaulu kwenda sekondari nilipohamia kwa walimu wa shule ya msingi Rwimbogo” Alisema Sprian.

Alisema hutumia vifaa ya kufundishia kutoka shule mama ya Rwimbogo  lakini hana mafunzo ya ualimu hivyo wakati mwingine hupata wakati mugumu wa kutumia mbinu za ufundishaji wanafunzi wa rika tofauti na mahitaji maalum.

Katika jengo hilo la  kanisa wanafunzi wanakalia vigoda na ubao unaotumika ni dari  huku kukiwa na vumbi na madirisha finyu ya kutolea mwanga na hewa, lakini pia huumba herufi kwa kuweka madaftari kwenye mapaja yao.

 Mwenyekiti wa kitongoji cha Bitunga Emanuel Elias alisema kutokana na changamoto ya ukosefu wa shule wananchi wameanzisha mkakati wa kukusanya vifaa vya kujenga shule katika kitongoji hicho.

 Alisema  wamekusanya mawe, Matofali na mchanga na tayari kumejengwa vyumba viwili vya madarasa na ofisi ya walimu ambavyo vimefikia hatua ya madirisha na kwamba kila mzazi anachangia Sh10,000 za  kulipa mafundi.
Alisema  wanafunzi hushindwa kwenda shule ya kijiji cha Mukalinzi ya Rwimbogo kutokana na umbali ambapo huanza utoro kuanzia majira ya mvua za vuli hadi masika zaidi ya miezi saba ya masomo na kwamba akitongoji hicho cheye kaya 294 kinao wakazi  2,352  wanaojihusisha na kilimo na ufugaji.

Hata hivyo Afisa elimu kata ya Muganza Mohamed Namtimba alisema Idara ya ukaguzi na wadhibiti ubora wa elimu wamefika kwenye kitongoji hicho kuruhusu ujenzi wa vyumba vya madarasa sita, matundu 16 ya vyoo na jengo la utawala.

Post a Comment

0 Comments