habari Mpya


Mama Ajifungua Vitu vya Ajabu,Wilayani Ngara.


Na Shaaban Ndyamukama,  RK –Ngara 97.9 fm.

 Wananchi wa kijiji cha Bulengo wilaya ya Ngara mkoani Kagera wamekumbwa na taharuki baada ya mwanamke mmoja wa kijiji hicho kujifungua mifuko ya plastiki mara tano ndani ya wiki mbili   ikiwa na vitu mbalimbali vya ajabu ingawa hakuna uthibitisho wa kitabibu kutoka kwa madaktari.

 Mwanamke huyo  Sara Daniel (22), ametajwa kujifungua makaratasi akiwa nyumbani kwa mumewe  katika kijiji hicho na kukuta vitu mbalimbali vinavyotishia usalama wa maisha yake huku akiwa na mimba ya  miezi minane.

Mwenyekiti wa kijiji cha Bulengo  wilayani Ngara Livingi John alisema jana kwamba baada ya kuapta taarifa za wanafamilia kuhusu mwanamke huyo kjifungua vitu vya ajabu alifuatiliaji kujiidhisha na kubaini ukweli wa tukio hilo.

John alisema baada ya kufika kwenye familia ya mwanamke huyo mumewe Josias Philmon alionesha mfuko wa plastiki  rangi nyeusi na ulipofunguliwa ulikutwa na msumari inchi tatu, fedha ya zamani ya East Africa iliyotobolewa katikati

Alisema vitu vingine ndani ya karatasi hiyo  kulikutwa mkaa vigawe vya vyungu, vipaande vya bati kama sufuria au sahani mawe na kokoto lakini kukiwa na vijiti viwili vilivyona karatasi yene ujumbe usemao “Tueshindwa labda wana madawa”

Leo ni mara ya nne akijifungua makaratasi hayo lakini haoneshi tumbo lake kupungua kutokana na ujauzito alio nao na sisi wananchi linatushagaza  na kuibua mtafaruku kwenye jamii wakilihusisha tukio na imani za ushirikina” Alisema John.

Akisimulia mkasa unaomkuta  Sara Daniel anasema alikuwa akisikia uchungu wa kujifungua akihisi kwenda haja ndogo na hutokwa na maji mengi sehemu za siri yanayoambatana na mifuko hiyo lakini hatokwi na damu wala kupata maumivu

Alisema kwa mara ya kwanza alianza kujifungua karatasi  Jumamosi ya Oktoba 5, mwaka huu na kuendelea hadi Hospitali ya Murugwanza kufanyiwa uchunguzi lakini ndani ya mifuko hiyo kulikuwa na vitu mbalimbali.

Naye Mume wa Sara  aliyejulikana kwa jina la Josias Philmon alisema hali hiyo imejitokeza  mwaka huu kwani tangu aishi na mke wake huyo wamejaliwa kupata mtoto mmoja na mimba moja kuharibika na hiyo aliyo nayo ni mimba ya tatu

 Alisema kutokana na mke wake kujifungua kwa njia ya kutatanisha nakutoa vitu vyenye kuwatia mashaka waliamua kwenda Hospitali ya Murgwanza lakini hakuna walichoambulia ispokuwa kurudishwa nyumbani baada ya siku tatu

Hata hivyo Mganga mkuu wa Hospitali ya Murgwanza Dr Remmy Andrew alikiri kumpokea Sara Daniel  na kuthibitisha  mama huyo kuwa na ujamzito wa miezi minane hivyo alipofanyiwa uchunguzi alikuwa hana mtoto tumboni.

Alisema serikali na kitaalamu hakuna imani za ushirikina hivyo anapaswa mama huyo na familia kuhakikisha anapata viini lishe vya kutuza mototo tumboni hadi afikishe umri wa miezi tisa na kumuwahisha zahanati atakapohitaji kujifungua.

Taharuki hiyo ya wanafamilia imeibua mjadala na kusababisha waumini kukusanyika na kufanya maombi huku wakichoma makaratasi hayo baadhi yao wakitaka kupiga kkura umaini anayesababsha hali  hiyo utokea.

Pamoja na hayo Viongozi wa Kijiji na Kata wakiongozwa na Diwani   wa Kata ya Mulukulazo Mhe.Mukiza Byamungu wamepinga maoni ya wananchi ya kupiga kura kumbaini mwenye kujihusisha na ushirikina ili kulinda amani ya familia na kijiji.

Post a Comment

0 Comments