habari Mpya


Walimu 10 Wastaafu Kibondo wapewa Mabati 180.

Katibu Tawala wa wilaya ya Kibondo Bw Ayubu Sebabili akimwakilisha Mkuu wa wilaya ya Kibondo Bw.Luis Bura akibidhi mabati 180 kwa walimu wastaafu 10 kwa niaba ya kamati tendaji ya Chama cha walimu Wilaya ya Kibondo (CWT)  kama zawadi kwa kufanya kazi iliyotukuka kwa kipindi chote cha utumishi wao katika ofisi za Chama cha waalimu CWT Wilayani Kibondo.

Picha/Habari Na James Jovin –RK Kibondo.
Chama cha Walimu (CWT) wilayani Kibondo mkoani Kigoma kimetoa mabati yenye thamani ya shilingi milioni 3 ikiwa ni bando moja la bati 18, kwa Walimu 10 waliostaafu hivi karibuni ikiwa ni sehemu ya kuwashukuru kwa kukitumikia chama hicho na serikali kwa uaminifu mpaka kufikia hatua ya  kustaafu.

 Akizungumza na Redio Kwizera muda mfupi baada ya hafla ya kuwakabidhi mabati hayo August 31,2018 Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu wilayani Kibondo Mwl. Ntiliyo Nzigo amesema kuwa utaratibu huo wa kutoa mabati kwa wastaafu ulianza tangu mwaka 2015 ambapo kila mstaafu hupewa bandari moja ya mabati.
Aidha amesema kuwa mabati hayo ni kwa ajiri ya Walimu waliostaafu kuanzia mwezi January mpaka March mwaka huu 2018 ambapo waliostaafu kuanzia mwezi April mpaka July mwaka huu, watakabidhiwa mabati yao mara baada ya fedha zao kutumwa kutoka makao makuu ya chama.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa wilaya ya Kibondo Bw Ayubu Sebabili akimwakilisha Mkuu wa wilaya ya Kibondo Bw.Luis Bura, kama mgeni rasimi katika hafula hiyo amewataka wastaafu hao kuyatumia mabati hayo kwa kujenga nyumba zitakazobaki kama kumbu kumbu na si kuyauza na kutumia fedha hizo kwa matumizi yasiyofaa.

Post a Comment

0 Comments