habari Mpya


Serikali yakabidhi Pikipiki 22 kwa Maofisa Elimu Kata Halmashaauri ya Wilaya Ngara.

Natamuka rasmi kwamba pikipiki ya Serikali haipotei wala kuibwa; itakayopotea au kuibwa ni pikipiki binafsi ya Afisa Elimu Kata.” Anasema Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara mkoani Kagera Bw. Aidan John Bahama.

Bw. Bahama ameyasema hayo wakati akipokea pikipiki 22 aina ya Honda, kofia ngumu 22 na ‘groves’ 22, vilivyopokelewa kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknojia Septemba 07, 2018 kwa lengo la kuwasaidia Mafisa Elimu Kata kusimamia ubora wa elimu katika Kata zao.
Aidha Serikali ya Tanzania imetoa pikipiki hizi kwa Maafisa Elim Kata, ili waweze kusimamia ubora wa elimu kupitia mpango wa kukuza stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu KKK na kufika kila kata kwa wakati ili kuinua kiwango cha elimu.

Kama zilivyo Halmashauri nyingine hapa nchini ambazo zilikuwa na tatizo la watoto wa shule za msigni kushindwa kusoma, kuandika na kuhesabu, Halmashauri ya Ngara nayo bado inachangamoto hiyo, lakini naamini pikipiki hizi zitakuwa msaada mkubwa katika kutokomeza tatizo hili.” Alisema Mkurugenzi huyo Mtendaji Bw. Bahama.

Pikipiki hizo ni mkakati wa Serikali katika kutekeleza sera ya elimu ya mwaka 2014, inayomtaka mtoto wa kitanzania amalizapo elimu ya msigi awe na maarifa, mahiri, na uwezo wa kuleta maendeleo yake binafsi na ya taifa.

Bw.Bahama ametoa rai kwa maafisa hao kuhakikisha wanavitunza na kwamba Serikali inatendelea kuboresha sekta ya elimu ili kuzalisha wataalamu watakaotumiwa kwenye uchumi wa viwanda.

Akifafanua jinsi usafiri huo utakavyowasaidia katika utendaji kazi wao,mmoja wa Afisa Elimu Kata ambaye jina lake limehifadhiwa, amesema pamoja na kufuatilia suala la KKK, bado atakuwa na nafasi ya kufuatilia masuala ya elimu, aliyoyataja kuwa ni maandalio ya masomo, mahudhurio ya wanafunzi na utendajikazi wa walimu katika shule za msingi na za sekondari katika kata zao.

Post a Comment

0 Comments