habari Mpya


Serikali Kigoma yaongeza Nguvu kuikabili Ebola.

Picha/Habari Na Adrian Eustus -RK Kigoma.

Serikali mkoani Kigoma imeendelea kukabiliana na uwezekano wa kuenea kwa virusi vya ugonjwa wa Ebola ulioripotiwa kushamiri katika nchi jirani ya Kongo DRC ambapo hadi sasa mkoa huo umetenga maeneo mbalimbali ya kupokea na kukagua wageni wanaingia na kutoka kupitia Bandari ya Kigoma baada ya meli ya MV Liemba iliyosimama kwa muda mrefu kuanza safari zake kutoka mkoani Kigoma kuelekea nchi ya jirani Zambia. 

Nahodha wa meli ya MV Liemba Bw. Titus Benjamini amesema kwa sasa kabla ya meli hiyo kuanza safari yake Abiria na Wafanyakazi wote wanapimwa kwa kutumia kifaa maalumu ili kubaini kama Hawana maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya Dkt. Leonard Subi ameutaka uongozi wa Bandari ya Kigoma sambamba na viongozi walioko maeneo ya mpakani kuhakikisha wanazingatia utaratibu wa kuwakagua watu wanaingia na kutoka nchini ikiwa ni pamoja na kuwashauri wafuate utaratibu wa kisheria kabla ya kutoka na kuingia nchini.

Meli ya MV Liemba iliyosimama kwa muda mrefu kuanza safari zake kutoka mkoani Kigoma kuelekea nchi ya jirani Zambia.

Post a Comment

0 Comments