habari Mpya


RC Kigoma Awataka Ma DC Kusimamia Vyema Zoezi la Vyeti vya Kuzaliwa.

Na Adrian Eustus -RK Kigoma.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga amewaagiza Wakuu wa wilaya za Mkoa huo kuhakikisha wanasimamia zoezi la uandikishaji na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ili kufikia wastani uliopangwa na serikali katika uandikishaji wa watoto ha.

Brigedia Maganga ametoa agizo hilo katika semina iliyowakutanisha viongozi mbalimbali wa serikali mkoani humo ambapo amesema takwimu za mkoa huo zinaonyesha watoto waliosajiliwa ni asilimia 8.1 ikiwa ni chini ya wastani kitaifa kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA ,Bi Emmy Hudson amesema Serikali imejipanga kuhakikisha watoto chini ya miaka mitano wanapatiwa vyeti vya kuzaliwa bila malipo na kwamba vitasaidia kutambua idadi ya watoto hao nchini.


Katika hatua nyingine, baadhi ya Madaktari kutoka Kamati ya kutokomeza Ugonjwa wa Polio wametoa tahadhali ya ugonjwa huo kwa Wananchi na kuwataka kutoa taarifa mapema katika vituo vilivyopo maeneo yao hali itakayosaidia kupunguza kasi ya kuenea kwa ugonjwa huo.

Post a Comment

0 Comments