habari Mpya


Mv Nyerere -Mazishi Jumapili September 23,2018, Idadi ya watu waliofariki yafikia 218.

Jeshi la Polisi wakishirikiana na Wananchi tayari wameshaanza kuchimba makaburi kwa ajili ya kuwapumzisha Marehemu waliofariki katika ajali ya MV Nyerere iliyotokea September 20,2018 katika wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza.

 Kwa Mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mhe.John Mongela ,idadi ya waliopoteza maisha mpaka sasa imefikia 218  huku maiti 171 zikiwa zimeshatambuliwa na ndugu zao kwa ajili ya mazishi.

Kesho September 23,2018 kuanzia saa 2 asubuhi shughuli ya mazishi ya Kitaifa itaanza.

Kivuko cha Mv Nyerere kilikuwa kikitoa huduma kati ya kisiwa cha Ukara na Bugorola wilayani Ukerewe.
Aidha Serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imetoa ufafanuzi kuwa Jumatatu  Septemba 24, 2018  ni siku ya kazi kama kawaida.

Baada ya Rais Magufuli kutangaza siku 4 za maombolezo kufuatia ajali ya MV Nyerere , kumekuwa na mkanganyiko kidogo  kwa baadhi ya watu kudhani Jumatatu itakuwa ni mapumziko.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Msigwa amesema Rais Magufuli alitangaza siku 4 za maombolezo  na sio siku za Mapumziko.

Msigwa ameandika;"Napenda kutoa ufafanuzi kuwa Jumatatu tarehe 24 Septemba, 2018 ambayo ni siku ya mwisho ya maombolezo ya Kitaifa, itakuwa ni siku ya kazi kama kawaida. Mhe. Rais Magufuli ametangaza siku 4 za MAOMBOLEZO na sio MAPUMZIKO."Post a Comment

0 Comments