habari Mpya


Ajifungua Katika Shamba la Miwa -Mkoani Kagera.

Na William Mpanju - RK Misenyi.

Wanawake Wajawazito wametakiwa kufika mapema katika Vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali hasa wanapokaribia kujifungua ili kuepuka kujifungulia njiani. 

Hayo yamesemwa  na muuguzi wa kituo cha afya Bunazi  Bi Blandina  Bahati  muda mfupi baada ya kumpokea  mwanamke mmoja  mkazi wa kijiji cha  Ibanga  kata ya Nsunga  wilayani  Missenyi  mkoani Kagera ambaye amejifungulia njiani wakati  akitembea  kwa mguu  kuelekea  kituoni hapo.

Bi  Lethicia  Didas
  akiongea na Radio Kwizera  mara baada ya kufika  kituoni hapo kupatiwa huduma   amesema  alipata uchungu  kabla  hajafika kituoni ndipo akalazimika  kujifungulia kwenye shamba la miwa  bila kuwa na msaada kutoka kwa wataalam tofauti na ndugu  yake aliyekuwa anamsindikiza. 
 
Nae Bi Peace  Elnest aliemsindika mama huyo amesema  chanzo  cha kujifungulia njiani  ni ukosefu wa fedha  ya nauli   ambapo  kutoka nyumbani  hadi  kufika  kituo cha afya  Bunazi ni umbali wa kilometa 15 na  usafiri wa pikipiki unagharimu  kiasi cha shilingi  elfu tano.

Post a Comment

0 Comments