habari Mpya


Adhabu ya Viboko yasababisha Wanafunzi kulalamika kwa DC Geita.

Na Gibson Mika -RK Geita.

Wanafunzi wa kidato cha tano na sita katika  shule ya sekondari ya Kalangalala iliyopo Mkoani Geita  wameandamana Jana August 31, 2018 majira ya asubuhi hadi ofisi ya Mkuu wa wilaya hiyo wakipinga kitendo cha kupewa adhabu kali shuleni ikiwemo adhabu ya  viboko.

 Hatua hiyo imekuja baada ya Mwalimu wa shule hiyo, aliyejulikana kwa jina moja ‘LAWI’ kudaiwa kumpiga mwenzao (JONATHAN MKONO)  hadi hatua ya kupoteza fahamu baada ya kukutwa bwenini wakati wa masomo.


Wakizungumza na radio kwizera baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wakiwa  nje ya ofisi ya mkuu huyo wa wilaya na mbele ya kamati ya ulinzi na usalama wamesema wanasikitishwa na kitendo cha mwenzao kupigwa hadi kupoteza fahamu na kwamba adhabu hiyo ya viboko imekuwa  ikitolewa mara kwa mara  kwa wanafunzi wote bila ya idadi.

Aidha Mkuu wa wilaya ya Geita Josephat Maganga amewataka wanafunzi hao kuwa watulivu na kwamba ataagiza timu yake kwenda kuchunguza swala hilo wakiwemo wadhibiti ubora wa elimu.

Aidha kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa Daniel Shila amekiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba upelelezi wa unaendelea.

Post a Comment

0 Comments