habari Mpya


ACACIA Kukamilisha Majengo ya Zahanati 32 Nyang’hwale.

Na Gibson Mika -RK Geita 90.5 FM.


Kushoto Anayesaini ni Mkurugenzi Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu na Buzwagi Bw.Benedict Busunzu , Kulia kwake  Ni Mkurugenzi wa Wilaya ya Nyang'hwale Bi Mariam Chaulembo.
Picha ya Pamoja ya Viongozi wa Mgodi, Viongozi wa Mkoa Ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robart Gabriel Pamoja na Viongozi wa Wilaya Nyang’hwale.Kufuatia upungufu wa vituo vya afya na zahanati katika wilaya ya Nyang’hwale Mkoani Geita,  Mgodi  wa Bulyanhulu kupitia kampuni ya ACACIA  uliopo mkoani Shinyang’a wameingia makubaliano na halmashauri ya wilaya hiyo katika ukamilisha wa majengo ya zahanati 32 ili kuwasaidia wananchi kupata huduma za matibabu .Akizungumza baada ya kutiliana saini na Uongozi wa Mgodi huo Mkuu wa mkoa wa Geita, Mhandisi Robart Gabriel amesema wamekubaliana na uongozi wa mgodi kutoa kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajiri ya ukamilishaji wa maboma ya zahanati katika vijiji 32 ili kuwasaidia wananchi kuepukana na changamoto ya kutembea umbali mrefu wakitafuta huduma za matibabu.


Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa ameutaka uongozi wa halmashauri hiyo kuweka utaratibu mzuri wa matumizi ya fedha hizo ili ziweze kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.
Balaza la Madiwani Nyang'hwale.Nae Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu na Buzwagi Bw, Benedict Busunzu amesema hatua hiyo itapunguza changamoto ya wananchi kutembea umbari mrefu wakitafuta huduma za matibabu na kuleta mapinduzi ya kimaendeleo hasa katika sekta ya afya.

Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi Mariam Chaulembo ameushukuru mgodi huo na kuhahidi kusimamia fedha hizo ili ziweze kakamililisha ujenzi wa maboma hayo kwa wakati na wananchi kuanza kunufaika na miradi hiyo.

Post a Comment

0 Comments