habari Mpya


Wazazi Sengerema washindwa Kuchangia Chakula cha Wanafunzi Shuleni.

Picha Na Maktaba yetu -Na Erick Ezekiel-RK Sengerema.

Halmashauri ya Sengerema Mkoani Mwanza imeshindwa kufikia lengo la Wananfunzi wote wa Shule za Sekondari za Serikali za kutwa kupata chakula shuleni kutokana na michango hafifu ya wazazi.

Hayo yamebainishwa na Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri hiyo Bw Godwin Barongo ambapo amesema Halmashauri ya Sengerema yenye jumla ya Shule 25 za Sekondari za Serikali kati ya shule hizo ni Shule 5 pekee zilizofanikiwa kuwa na chakula cha mchana kwa kwa Wanafunzi wake.

Amesema kuwa mpango wa kutoa chakula cha mchana shuleni ni kudhibiti utoro kwa wanafunzi licha ya kwamba bado kuna wazazi ambao hawajawa  na uelewa wa jambo hilo.

Akizungumzia  mwitikio wa wazazi kuchangia chakula cha wanafunzi  shuleni amesema mwitikio  bado ni hafifu kutokana na jamii kuwa na dhana   ya  elimu   bila malipo na kwamba upo mpango wa kuweka  sheria ya kuchangia kwa nguvu  chakula  hicho.

Kwa  upande  wao  baadhi  ya  wananchi   wamesema   wako tayari    kuchangia chakula   kwani ni  muhimu kwa wanafunzi shuleni   kwakuwa kitawasaidia  kusoma katika mazingira rafiki wakiiomba serikali kuwachukulia hatua kali  walimu watakaobainika kujinufaisha na chakula   hicho.

Post a Comment

0 Comments