habari Mpya


Wanakagera Naombeni Ushirikiano kuwaletea Maendeleo -RC Kagera.

Na: Sylvester Raphael.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti akabidhiwa rasmi Ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu katika hafla fupi iliyofanyiaka katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Agosti 6, 2018. 

 Aidha, mara baada ya kukabidhiwa ofisi Mkuu wa Mkoa Mhe. Gaguti alimwapisha Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Rashidi Mohamed Mwaimu.

Mara baada ya kukabidhiwa Rasmi Ofisi Mkuu wa Mkoa Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti ambaye sasa anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera wa 23 tangu uhuru mwaka 1961 alimshukuru mtangulizi wake Mhe. Kijuu na kuhaidi kutomwangusha kwa juhudi zake alizozifanya katika kuleta maendeleo ya Mkoa wa Kagera.
Nihaidi wananchi wa Mkoa wa Kagera Utumishi uliotukuka pia nikuhaidi Mzee wangu Mhe. Kijuu kuwa nikiwa hapa Mkoani Kagera kama Mkuu wa Mkoa nitahakikisha naendeleza juhudi zako zote ulizokuwa ukizifanya kuwaletea maendeleo wananchi wa hapa Kagera, kikubwa nitaomba ushirikiano mkubwa kutoka kwao,” Alifafanua Mhe. Gaguti.

Mambo Muhimu ambayo Mhe. Gaguti amehaidi kuyafanyia kazi yeye kama Mkuu mpya wa Mkoa wa Kagera ni Kudumisha Ulinzi na Usalama wa Mkoa hasa katika mipaka na nchi jirani kwa kudhibiti magendo ya mazao hasa kahawa, kudhibiti uingizwaji wa mifugo katika Misitu ya Akiba na Hifadhi ambayo sasa Serikali imeyatangaza kuwa hifadhi za Taifa.

Pia Mhe. Gaguti alisema atahakikisha kuwa fursa ya kuwa na mipaka na nchi jirani inatumika ipasavyo ili kuinua uchumi wa Mkoa wa Kagera kwa wananchi kufanya biashara na nchi jirani ili kujiongezea kipato na kunufaika na mipaka ya nchi zinauzunguka Mkoa wa Kagera.
Naye Mkuu wa Mkoa aliyemaliza muda wake Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu mara baada ya kukabidhi ofisi rasmi akitoa neno la kuwaaga wananchi wa Kagera alisema kuwa anamshukura Rais John. Pombe Magufuli kwa kumkubalia kustaafu ili akapumzike.

 Aidha, aliushukuru uongozi wa mkoa pamaoja na wananchi wa Kagera kwa ushirikiano waliompatia wakati akitekeleza majukumu yake na kuwaomba pia ushirikiano huo waendelee kumpatia Mhe. Gaguti.

Wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Askofu Msaidi wa Jimbo Katoriki la Bukoba Methodius Kilaini wakimuaga Mkuu wa Mkoa Mstaafu Mhe. Kijuu walimtakia maisha mema katika mapumziko yake, aidha, walimshukuru kwa kuuvusha Mkoa wa Kagera katika kipindi kigumu hasa wakati wa Tetemeko la Ardhi lililotokea Septemba 10, 2016.

Post a Comment

0 Comments