habari Mpya


Wainjilisti wanane Kanisa Anglikan Dayosisi ya Kagera Wapatia Daraja la Ushemasi.

Mashemasi.

- Na Shaaban Ndyamukama.

Kanisa kuu  la Anglikan  dayosisi ya Kagera limewasimika wainjilisti wanane wa kanisa hilo kwa kuwapatia daraja la ushemasi na kuwasimika viongozi 11 wa Ushirika wa Mwanamke Kikristo (UMAKI) kusaidiana na askofu kuongoza kanisa na waumini wake katika parishi mbalimbali ndani ya dayosisi hiyo.

Akiwasimika Mashemasi na Viongozi wa UMAKI, Askofu wa Kanisa hilo Darlington Bendankeha amewahimiza kuwa kiungo kati ya kanisa  na waamini kwa kujenga upendo amani na mshikamano katika mafundisho yaliyo na  madili ya kiroho na jamii kwa ujumla.
Viongozi wa UMAKI.

Askofu Bendankeha  amesisitiza waumini kufuata maandiko matakatifu ya biblia na viongozi ya kanisa kushirikiana pamoja na mashemasi hao kulijenga kanisa kwa kuongeza ukusanyaji wa sadaka, kuhimiza ufungaji wa ndoa takatifu, kuongeza uchumi wa kila parishi na familia zao .

"Waumini nawapeni wito wa kuwapokea mashemasi hawa kwa kuwaelekeza na kusikiliza mafundisho yao wakilenga kuwakomboa watu wenye mahitaji kama yatima walemavu wanawake wasiojiweza na kuanzisha miradi ya kiuchumi" Alisema Askofu .
Ibada ya kuwasimika viongozi hao imehudhuriwa na  Askofu mstaafu wa kanisa hilo Dr AARON KIJANJALI wakiwemo wachungaji kutoka Uingereza na wengine wa ndani ya dayosisi hiyo, waamini ambapo katika kula kiapo mashemasi na viongozi wa UMAKI wameahidi kufuata taratibu, kanuni na sheria za kanisa katika kutimiza wajibu na majukumu yao.

Wakati ibada hiyo ikifanyika Mwinjilisti wa Kanisa la Anglikana kutoka kijiji cha Ngundusi kata ya Kabanga wilayani Ngara Scott Edward ambaye amepata daraja la kuwa Shemasi katika kanisa kuu la Anglikan Murugwanza amelipokea huku akiwa na huzuni kubwa baada ya nyumba ya familia yake kuungua moto.
 
Hayo yamebainishwa na Vicar General wa dayosisi ya Kagera Furaha Kamana  wakati wa ibada ya kuwawekea mikono mashemasi wapya ambao walikuwa wainjilist kutoka parish mbalimbali wa dayosisi hiyo ilifanyika kanisa kuu la Murugwanza wilayani Ngara.
Furaha Kamana amesema shemasi hiyo ambaye mkazi wa Kitongoji cha mukitamo kata ya kabanga wilayani humo alipata taarifa za kuunguliwa nyumba yake juzi SAA za usiku na mazao, mavazi na mali nyingine ziliungua kabisa ikiwa ni pamoja na nyumba kuanguka kuta licha ya kujengwa na kuezekwa kwa bati.

"Tulifika saa tano za usiku eneo la tukio tulichokutana nacho ni moshi na moto mkubwa ukitanda kukiwa na harufu ya vitu vilivyoungua maana  kila kitu kiliteketea  wakati yeye na mkewe wakiwa kwenye mafunzo ya nadhili ya daraja hilo" Alisema Kamana

Hata hivyo kufuatia taarifa hiyo ya kusikitisha na kuhuzunisha, waumini wa kanisa hilo wamemchangia vitu mbalimbali ili kuanza maisha mapya huku akihimizwa kujenga ujasiri wa moyo wake na kwamba hayo ni majaribu kwake katika kulitumikia kanisa la Mungu. 

Post a Comment

0 Comments