habari Mpya


Kagera kupokea bilion 4.5 kwaajili ya ujenzi wa Hospitali za wilaya

Pichani aliyesimama ni mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera Luten Kanali Michael Mtenjele akisoma taarifa ya afya ya mkoa wa Kageera kwa Waziri wa afya,jinsia ,wazee na watoto Bi.Ummy Mwalimu kwa niamba ya Mkuu wa mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marico Gaguti.


Picha na Samuel Lucas

Story na   Julius Njole
Mkoa wa Kagera unatarajia kupata shilingi bilioni 4.5 kwa mwaka huu wa fedha  kwaajili ya ujenzi wa hospitali mpya za wilaya ambazo zitajengwa katika wilaya za Karagwe, Bukoba na Kyerwa.
Pichani ni Waziri wa afya,jinsia ,wazee na watoto Bi.Ummy Mwalimu akiwasili Rusumo wilayani Ngara mkoani Kagera.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Marco Gaguti katika taarifa mkoa kwa waziri wa afya,maendeleo ya jamii jinsia,wazee na watoto Bi.Ummy Mwalimu ambayo imesomwa na mkuu wa wilaya ya Nagra Luteni Kanili Michael MtenjelePichani ni Waziri wa afya,jinsia ,wazee na watoto Bi.Ummy Mwalimu baada ya kuwasili Rusumo wilayani Ngara mkoani Kagera akipokea taarifa kutoka kwa Stanley Chipasula mtoa huduma za afya katika kituo cha kupima raia wa kigeni wanaoingia nchini kupitia mpaka wa Rusumo.


Taarifa hiyo imesema mpaka sasa umefanyika ukarabati wa vituo vya afya 4 vya Kimeya ,Naykanazi, Mabawe, Murusagamba, Katoro, Kashanje, Kayanja na Murongo vilivyo gharimu bilioni 3.5.

Dakt.Chipasula akipokea maelekezo kutoka kwa waziri Ummy Mwalimu.
Bw.Gaguti ameongeza kuwa mkoa umepata shilingi bilioni 2.4 za ukarabati wa vituo 6 vya  Nyakayanja, Naybusozi, Maruku, Kamuli, Zamzam na Bunazi ambapo kila kituo kimepatiwa shilingi milioni 400.


Pichani juu ni banda maalum kwaajili ya shughuli zakuwapumzisha Raia wanao onekana na dalili za ugonjwa Ebola


Pichani juu ni Waziri wa afya,jinsia ,wazee na watoto Bi.Ummy Mwalimu akikagua banda maalum kwaajili ya shughuli zakuwapumzisha Raia wanao onekana na dalili za ugonjwa Ebola.
Pichani juu ni Waziri wa afya,jinsia ,wazee na watoto Bi.Ummy Mwalimu akijibu maswali ya wandishi wa habari waliokuwa katika ziara hiyo.


Pichani juu ni Waziri wa afya,jinsia ,wazee na watoto Bi.Ummy Mwalimu akitoka kwenye kikao cha ndani na kamati ya ulinzi na usalama kilichofanyika katika eneo la Rusumo

Pichani juu ni Waziri wa afya,jinsia ,wazee na watoto Bi.Ummy Mwalimu akiagana na mkuu wa wilaya ya Ngara Luten Kanali Michael Mangwela Mtenjele tayari kwa kuelekea jijini Dodoma.
Pichani juu ni mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera  Luten Kanali Michael Mangwela Mtenjele akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama wilaya baada ya waziri Ummy kuondoka


Post a Comment

0 Comments