habari Mpya


Muonekano wa Rusumo sasa Ulivyo Baada ya Ajali ya Moto August 19,2018.

Mabaki ya magari 6 na trekta moja yaliyoteketea kwa moto August 19,2018 katika kituo cha Forodha cha Rusumo kinachounganisha Nchi ya Tanzania na Rwanda,mpaka uliopo Wilaya ya Ngara mkoani Kagera baada  ya Lori la Mafuta kupoteza mfumo wa breki na kuyagonga magari mengine yaliyokuwa yakisubiria utaratibu wa kuvuka mpakani kisha moto kulipuka na kusababisha mengine kupatwa moto huo.

Picha Na Maria Philbert - RK Ngara.

Waandishi wa Kituo cha Radio Kwizera cha wilayani Ngara,Samwel Lucas na Feliciana Manyanda wakiongea na mmoja wa Dereva ambaye gari lake liliteketea kwa moto katika tukio hilo.

Aidha hadi sasa Mkuu wa Wilaya Ngara Luteni Kanali Michael Mtenjele amesema  Halmashauri ya wilaya hiyo haina uwezo wa kununua gari la Zimamoto kwa ajili kuzuia majanga yanayotokana na moto kwani mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo hayajitoshelezi.
Waandishi wa Kituo cha Radio Kwizera cha wilayani Ngara,Njohore na Feliciana Manyanda wakiongea na Kiongozi wa Zimamoto mkoani Kagera kuhusu changamoto mbalimbali walizonazo kuhusu namna ya kukabili majanga ya moto mkoani Kagera.

Post a Comment

0 Comments