habari Mpya


Mbunge wa Ngara Ashindwa Kuzindua Mradi wa Maji Shule ya Sekondari ya Wasichana Baramba kutokana na Kukosa Umeme wa Uhakika.

Mbunge wa jimbo la Ngara mkoani Kagera Mhe.Alex Gashaza  Akizindua Mradi wa Maji wa Shule ya Sekondari ya Wasichana na Baramba ,wilayani Ngara mkoani Kagera.

Pichani Mbunge huyo akifungua Bomba ambalo Hata hivyo lilishindwa kutoa Maji kutokana na huduma hiyo ya Maji kutopatikana.

 Picha/Habari -Na Shaaban Ndyamukama –RK Ngara.
Mbunge wa Jimbo la Ngara mkoani Kagera Mhe. Alex Gashaza  leo August 17, 2018 ameshindwa kuzindua mradi wa maji wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Baramba wilayani Ngara baada ya kuwempo Ukatikaji wa  nishati ya umeme  mara kwa mara katika  wilaya hiyo.

 Mhe.Gashaza alikuwa akizindua mradi huo uliofadhiliwa na Shirika la Marafiki wa Afrika kwa thamani ya Shilingi Milioni 130  ambapo hii leo ikiwa  ni maadhimisho ya miaka 20 ya kuanzishwa kwa Shirika hilo wilayani Ngara tangu mwaka 1997 kutoa huduma za kijamii.

Mwenyekiti wa Shirika la Marafiki wa Afrika Tanzania Padre Isias Bambara amesema kukatika kwa umeme umekuwa ni changamoto ya maendeleo  kwa wanafunzi wa shule hiyo ambao ni moja ya mradi wa shirika hilo wilayani Ngara

Amesema Shirika la MAT lilianza mwanzoni mwa mwaka 1981 chini ya  wamisionari wa kikatoliki kutoka nchini Ujerumani likishirikiana na mapadre wa jimbo la Rulenge wakati huo  wakiongozwa na marehemu  Askofu Christopher Mwoleka kueneza injili ya jumuia ndogondogo jimboni humo.

Pia amesema Shirika la Marafiki wa Afrika linashirikiana na mashirika mengine hapa nchini ya TWAWEZA,TACAIDS, NELSAP,na TASAF chini ya ufadhili wa Shirika la Marafiki wa Afrika Ujerumani, Red Charity na Serikali ya Tanzania.
Hata hivyo Mbunge ameridhia kuendelea na shughuli nyingine  katika sherehe hizo ambazo zimehudhuriwa na watu mbalimbali kupata taarifa za miradi ya kijamii hasa katika sekta ya elimu afya maji na ujasiliamali katika mkoa wa Kagera.

Baada ya zoezi hilo kukwama Mhe.Gashaza aliendelea na shughuli nyingine kupata taarifa za utekelezaji wa miradi  ya maendeleo ya kijamii  huku akikata utepe wa mnara wa kumbukumbu wa marafiki wa afrika tangu kuanzishwa na kupata usajili mwaka 1997 katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Baramba wilayani Ngara.

Amesema kukatika kwa umeme wilayani Ngara  baada ya kuingia katika mfumo wa gridi ya Taifa unasababishwa na kiwango kidogo kinachotoka katika kituo cha gridi ya taifa wilayani Biharamulo hivyo kushindwa kuhimili mahitaji ya wananchi

Aidha amewashukuru waanzilishi wa marafiki wa Afrika Tanzania na Ujerumani na kuisaidia jamii ya mkoa wa Kagera kwa kusaidia kupatikana shule pekee ya Sekondari Wasichana wilayani Ngara yenye kulenga ukombozi wa mtoto wa kike kitaaluma na kupata wataalamu wenye kuleta mapinduzi ya kutokomeza umaskini.
Amesema eneo ilipo shule ya wasichana Baramba makao makuu ya marafiki wa Afrika  limenufaika na kituo kidogo cha Afya kwa ajili ya wananjamii, na pamejengwa taasisi  kama kituo cha JWTZ  ikiwemo shule ya sekondari ya wavulana Lukole inayochukua wanafunzi wa kidato cha tano.

“Tunapoadhimisha  miaka 20 ya MAT wananchi tujitahidi kutunza miun dombinu iliyogharimu malilioni ya fedha zaidi ya Sh572 milioni kwa wilaya ya Ngara na Sh102 milioni kwa wilaya ya karagwe na kunufaika nayo” Amesema Gashaza

Amewakaribisha wafadhili kutoka Ujerumani kuwekeza miradi mbalimbali mkoani kagera kwa kutumia vivutio mbalimbali kwa kufanya utalii wa ndani utamaduni wa kijadi utengenezaji wa bidhaa za asili na kuongeza uzalishaji kiuchumi.

Shirika la Marafiki wa Afrika Tanzania limetoa ufadhili  wa kuwasomesha watoto 85 yatima katika wilaya ya Ngara  mkoani Kagera  kwa kugharimia mahitaji ya kielimu kwa thamani ya Sh116 milioni kati ya mwaka 1997 hadi mwaka jana 2017 tangu kuanzisha miraji ya kijamii mkoani humo.

Katibu mtendaji wa Shirika hilo  David Bukozo ametoa taarifa hiyo Agost 17 katika maadhimisho ya jubilee ya miaka 20 ya kuanzishwa shirika la Marafiki wa Afrika Tanzania  (MAT) yaliyofanyika  shule yasekondari ya wasichana Baramba wilayani Ngara.

Bukozo amesema sanjari na ufadhili kwa  watoto hao shirika hilo limetumia Sh102.6 milioni kufadhili miradi ya elimu, kilimo,afya,ufugaji, elimu ya ufundi kwa vijana, wanawake wajane kabla na baada ya kusajiliwa katika  wilaya ya Karagwe na kuanzisha miradi hiyo wilayani Ngara.

Amesema miradi mingine iliyoanzishwa na kuendelezwa wilayani Ngara ya elimu Afya kilimo ufundi na ujasiliamali kwa vikundi vyenye watu wa rika mbalimbali viligharimiwa Sh455.8 milioni  na kuwawezesha kujipatia maendeleo.

"Mbali na fedha za kugharimia miradi hiyo  marafiki wa Afrika kutoa Ujerumani walisambaza  vifaa vya ufundi , dawa na  vifaa tiba katika taasisi mbalimbali wilayani  Ngara na kunufaisha wanajamii kupata maendeleo”Amesema Bukozo.

Amesema baada ya kuungana  na kuanzisha ushirika wa kichungaji mwaka 1997 walianzisha umoja huo kwa mikataba ya kulenga kutoa huduma za kijamii katika sekta ya elimu, Afya, Maji, na kuwezesha watoto yatima na wanaotoka mazingira magumu kupata njia za kuwakwamua na changamoto za maisha.

Post a Comment

0 Comments