habari Mpya


Mafanikio ya Maktaba zinazojengwa na Jambo Bukoba wilayani Ngara.

Meneja Miradi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Jambo Bukoba la Mkoani Kagera Bw.GONZAGA STEVEN (kushoto) akimkabidhi Picha ya Ukumbusho ya Wafadhili wa Mradi wa Ujenzi wa Maktaba katika Shule ya Msingi Buhororo wilayani Ngara Mwalimu Mkuu, Mwl.MASUMBUKO BWIRE Jana August 20/2018. 

Maktaba hiyo yenye Vitabu mbalimbali vya kiada na ziada imejengwa kwa fedha za wafadhili WERNER & KARIN kupitia JAMBO BUKOBA shilling milioni 4 na Mchango wa Jamii shilingi milioni 4.

Wanafunzi wa Darasa la Saba wakijisomea Kitabu cha Sayansi darasani  wakipata urahisi wa Vitabu kutoka katika Maktaba ya Shule yao ya Msingi Buhororo wilayani Ngara.

Post a Comment

0 Comments