habari Mpya


Kahama Kukusanya Uchafu kwa Mfumo wa Kisasa Zaidi.

Mrundikano wa Uchafu-Picha na Maktaba yetu.

Halmashauri ya mji wa Kahama Mkoani Shinyang’a inatarajia kubadilisha mfumo wa ukusanyaji wa Takakata baada ya kuwepo kwa ongezeko la uzalishaji wa taka   jambo linalochangia mzabuni anaefanya kazi hiyo kushindwa kufikia malengo.

Akizungumza na Radio Kwizera Mkuu wa Idara ya  ya usafi na Mazingira katika Halmashauri ya mji  wa Kahama Bw Martine  Masele amesema mfumo wa ukusanyaji wa taka utabadilika na badala ya kutumia mzabuni watatumia vijana ili kuwajengea uwezo wa kupata kipato.

Bw Masele amesema kuwa halmashauri ya mji wa Kahama kumekuwepo na ongozeko la uzalishaji wa taka tani 121 hadi tani 137 jambo linalochangia mzabuni kushindwa kuzikusanya kwa siku na kuufanya mji kuendelea kuwa mchafu.

Kutokana na hali hiyo halmashauri itagawiwa kwenye kanda nne ambapo wakusanyaji wa taka itakuwa ni rahisi kuzifikia taka na kwamba asilimia 80 ambayo mzabuni alikuwa akipokea zitakwenda kwa vikundi vya vijana walioko kwenye kanda hizo na kwamba hali hiyo itawasaidia kupata kipato kipitia ukusanyaji huo 

Post a Comment

0 Comments