habari Mpya


Gari la Waziri wa Afya (Ummy Mwalimu) lasababisha Ajali –Kahama.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi.Ummy Mwalimu akiwasili  Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera August 27, 2018 wakati wa ziara ya siku moja  katika mpaka wa Tanzania na Rwanda  eneo la Rusumo wilayani Ngara ili kuangalia ni kwa jinsi gani mkoa wa Kagera umejipanga kudhibiti ugonjwa wa homaya Ebola.
Gari (la kwanza pichani kushoto ) lililombeba Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi.Ummy Mwalimu  limepata ajali na kumgonga mwendesha Baiskeli na kumsababishia majeraha mwilini mwake.

Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga Simon Haule amesema gari hilo lenye namba za usajili  STL 2777 Mali ya Wizara ya Afya likiendeshwa na Dereva Bw. Jumanne Ally amemgonga Marko Charles mkazi wa kata ya Busoka katika Halmashauri ya mji wa Kahama.

Amesema Waziri Ummy alikuwa akitokea wilayani Ngara kwenye ziara ya kikazi ya siku moja na kwamba Bw. Marco aliegongwa amepata majeraha kwenge bega na mkono wa kushoto na amelazwa hospitali ya mji wa Kahama.

Hata hivyo Kamanda Haule amsema baada ya ajali hiyo dereva ameruhusiwa kuendelea na safari kwani Waziri anaelekea Dodoma kikazi na uchunguzi bado unaendelea kwani ikithibitika dereva alifanya uzembe atafikishwa Mahakamani.

Post a Comment

0 Comments