habari Mpya


DED Misenyi - Ataka Wanyeviti kuitisha Mikutano ya Hadhara kwa Maendeleo ya Wananchi.

Babu na Bibi wa Misenyi mkoani Kagera wakisikiliza Kwa makini moja ya Mkutano wa Hadhara –Picha na Maktaba yetu.

Na Wiliam Mpanju –RK Misenyi.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Missenyi  mkoani  Kagera  Bw  Limbe  Benard  amewaagiza wenyeviti wa vijiji na vitongoji kuitisha mikutano ya hadhara  ili  kusikiliza kero za wananchi na kuwasomea mapato na matumizi.

Bw Benard amesema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kasambya kwenye mkutano Wa hadhara juu ya ushirikishwaji wa wananchi katika kuibua miradi ya kimaendeleo.

Amesema wenyeviti wanashindwa kuitisha mikutano kwa ajili ya kuzungumzia masuala mbalimbali ya maendeleo yao hasa kuwashirikisha wananchi katika kuibua miradi hiyo.

Nao baadhi ya Wenyeviti wa Vijiji  na Watendaji  wamesema  changamoto kubwa ni wananchi kushindwa kuhudhuria mikutano inapoitishwa hivyo  kukwamisha mikutano  na kueleza kuwa wanaendelea kuhamasisha wananchi  juu ya wajibu wao kushiriki mikutano hiyo kwa manufaa ya maendeleo yao.

Post a Comment

0 Comments