Jumla ya
Shule 18 za Sekondari wilayani Ngara mkoani Kagera zimepata Vifaa vya Michezo
vitakavyosaidia kuleta maendeleo ya michezo katika shule zao.
Vifaa hivyo
vilivyotolewa na Kampuni ya Vinywaji baridi ya Coca-Cola ni pamoja na Jezi seti
moja kwa wavulana na wasichana, mpira wa soka na kikapu mmoja kwa kila shule.
Mbunge wa
Jimbo la Ngara Mhe.Alex Gashaza amekabidhi vifaa hivyo Jana August 2, 2018
katika ofisi za Idara ya ya Michezo na Utamaduni wilayani Ngara, hafla
iliyohudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Mhe Erik
Nkilamachumu na Wakuu wa Shule zote 18 za Sekondari. |
0 Comments