habari Mpya


WAWATA Jimbo Katoriki la Rulenge Ngara Wasaidia milioni 14 Wanafunzi wa Shule ya Seminary Katoke.

Na –James Jovin –RK Biharamulo.

Wanawake Wakatoriki Tanzania WAWATA Jimbo Katoriki la Rulenge Ngara na Dekaniya ya Chato wametoa Vitu vyenye thamani ya Shilingi Milioni 14 na Laki Saba kwa Wanafunzi wa Shule ya Seminari Katoke iliyoko wilayani Biharamulo mkoani Kagera  ikiwa ni sehemu ya kunyonyesha wanafunzi hao na kulea miito ambapo kufanya hivyo ni wajibu wa kila mwanakanisa .

Shughuli hiyo imefanyika siku ya jumamosi July 21, 2018 shuleni katoke ambapo WAWATA kutoka  parokia zote za Jimbo Katoliki Rulenge ngara walifika na kutoa vitu mbali mbali ikiwemo mahindi,maharage ,mchele na vinginevyo ikiwa ni utamaduni wao wa kunyonyesha wanafunzi hao kila mwaka mara moja.

Paroko wa Parokia ya Ngara mjini Padre Sixmundi Nyabenda  ambaye alikuwa MC katika shughuli hiyo amewapongeza WAWATA kwa moyo wao wa kutoa kwani vitu hivyo vitasaidia kwa kiasi kikubwa kuwalisha wanafunzi hao na kwamba awamu hii wametoa kiasi kikubwa ukilinganisha na mwaka jana.                 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa WAWATA jimbo la Rulenge Ngara Bi Bronia Philmon  akisoma risara iliyoandaliwa na kamati tendaji ya Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa kamati hiyo Padre Adrian Kayunkilwa amesema kuwa mafanikio ya mwaka huu ambapo ni awamu ya sita  yametokana na mikakati mipya iliyowekwa mwaka jana.  

Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara Sevelin Niwemugizi ambaye alikuwa mgeni rasimi katika shughuli hiyo ya WAWATA amesema kunyonyesha ni sehemu ya wajibu wa kulea miito ambapo wajibu huo ni wa kila mwanakanisa katika kuiendeleza imani katoliki.

Post a Comment

0 Comments