habari


Wakulima wilayani Muleba:Tunashindwa kunufaika na kilimo kwasababu hatuna wataalam wa kilimo wa kutosha.

MULEBA: NA SHAFIRU YUSUFU
Imeelezwa kuwa sababu inayopelekea wakulima wilayani Muleba Mkoani Kagera kutonufaika na Kilimo chao inatokana na uhaba wa watalaamu wa kutosha wa Kilimo ili kutoa elimu ya kutosha kwa wakulima na kuachana na Kilimo cha mazoea.

Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa mafunzo ya uendeshaji na matunzo tume ya taifa ya umwagiliaji Bw.Petrol Sarwat  wakati akizungumza na wakulima wa zao la Mpunga katika Kijiji cha Kyota Kata ya Kimwani na kuwapatia elimu juu ya Kilimo cha umwagiliaji cha zao la  Mpunga.
Kwa upande wao baadhi ya wakulima waliokuwa kwenye mafunzo hayo wamesema pamoja na kukosa elimu Kutoka kwa  wataalamu wa kilimo bado soko la uhakika limekuwa kikwazo kikubwa hali inayopelekea kushuka kwa thamani ya mkulimaPost a Comment

0 Comments