habari Mpya


Wakulima wa zao la Kahawa fuateni ushauri wa kuvuna kahawa iliyokomaa kwaajili ya faida yenu

Na Shaaban Ndyamukama RK Ngara
Wakulima wa zao la kahawa katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera wametakiwa kusikiliza na kufuata ushauri wa serikali wa kuvuna Kahawa iliyokomaa ili iweze kuwaongezea mapato kwenye soko la dunia.


Ushauri huo umetolewa na mmoja wa wakulimawa kijiji cha Buhororo wilayani Ngara Odas Mathayo, wakati akiongea na mwandishi wa habari hii shambani kwake wakati akivuna zao hilo   hii leo kwa kuchambua mbegu iliyowiva.

Odas Mathayo amesema amatarajio yake ni kuvuna kahawa aina ya Robosta kilo 400 baada ya kupanda miche 300  ndani ya shamba lenye ukubwa wa ekari moja tangu alianzishie kilimo cha kahawa mwaka 2010 kijijini hapo.

Amesema kilimo cha Kahawa kinazo changamoto za kiutendaji hasa kutendea shamba kwa kutandaza Nyasi, kukata vikonyo katika matawi ya mmea na kuvuna mbegu iliyo nyekundu kwa kuanika pia kuanua  juani

“Nimeishafaidiaka na kilimo cha kahawa baada ya mavuno sababu ninapata matumizi ya familia na kuwasomesha watoto lakini kwa sasa nimeboresha maisha kwa kujenga nyumba bora” Amesema Odas Mathayo 

Pamoja na hayo amesema hajawahi kutembelewa na maafisa kilimo kumuelekeza jinsi ya kuboresha shamba lake ispokuwa ujuzi huupata kwa wakulima wenzake kijijini humo na vijiji jirani huku akiwataka vijana kujihusisha na kilimo hicho.


Wakati huohuo mkulima wa kijiji cha Muhweza Salvatori Misago yeye amekuwa tofauti na mkulima wa Buhororo kwa kuvuna kahawa mbichi na kuianika akidai imeanza kushambuliwa na jua ambayo ni aina ya arabika
Amesema kahawa hiyo ikishawakiwa jua tunda lake au mbegu haiwezi kuonekana  nyekundu licha ya kukomaa hivyo inavunwa hivyohivyo na kwamba hakuweza kuianika kwenye chanja kwa sababu ni gharama
Ukitaka kuianika kwenye chanja lazima kukata miti ambayo sina lazima kuinunua, kukata nyasi na makuti ya migomba, lakini lazima kuweka shitingi ambalo kulipata lazima linunuliwe” Amesema Misago

Serikali ya mkoa wa Kagera imezindua msimu wa kuuza kahawa ambapo mkulima atatakiwa kupeleka zao hilo kwenye chama cha ushirika ikiwa ya maganda safi bila takataka yoyote na kulipwa kianzio cha Sh1000 kwa kilo moja.Mwisho. 

Post a Comment

0 Comments