habari Mpya


Waislamu Kagera kuweni Makini na Matapeli wakati wa Maandalizi ya Hijja.

 Muonekano wa Masheikh ,Mahaji na Mahajati waweka mikakati ya kujiandaa kwenda hija na kuwatahadhalisha Waislaam kuwa Makini na Makampuni na Taasisi binafsi wanaochukua tenda ya kuwasafirisha mahujaji ambao wanawatapeli kwa kuwakatia viza feki na kupelekea kukwamisha safari zao za kwenda kutimiza moja ya nguzo 5 ya dini ya kiiislam mjini Maka, nchini Saud Arabia.

Na –Wiliam Mpanju RK Missenyi. 
Imam Mkuu wa Msikiti wa Kagera Sugar wilayani Misenyi mkoani Kagera , Sheikh Ally Khamis  akitoa neno katika kikao cha ufunguzi wa umoja wa Masheikh,Mahaji na Mahajati wa wilaya za Misenyi,Kyerwa,Karagwe na Bukoba Vijijini uliofanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari Kabwoba wilayani Misenyi, amesema kuwa wanaosimamia Mahujaji wanatakiwa kuwa wachamungu ambapo baadhi ya Waislam wamekuwa wakishindwa kufika MAKA baada ya kutapeliwa hivyo kukwamishwa safari yao kutokana  na watu hao kuwa na tamaa ya kupata mali kwa njia ya utapeli . 
 Baadhi ya Waislam waliohudhuria hafla hiyo,Wamesema kuundwa kwa umoja huo kutawezesha Waislaam kujengeka katika misingi ya uislaam kwa kusaidiana katika shida na raha kama sehemu ya kujenga mshikamano baina ya waislam.

Kwa upande wake,Katibu wa Baraza kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA mkoani Kagera Sheikh Abdumarick Mwijage aliyemwakilisha Sheikh wa mkoa wa Kagera,amesema kuwa umoja huo utawasaidia Waislamu wengi kupata elimu ya hija na hivyo kuwasihi Mahaji,Masheikh na Mahajati kujitokeza kwa wingi ili kujiunga na umoja huo.
 

Post a Comment

0 Comments