habari Mpya


Vijana fungeni ndoa takatifu kama Sehem ya kufanya Ibada

MWANZA NA.SHAABAN NDYAMUKAMA.
Vijana waliopevuka wenye kuanzia umri wa miaka 20 na kuendelea hapa nchini wameshauriwa kujihusisha kutenda  ibada ya kufunga ndoa takatifu katika  imani za kiroho.

Ushauri huo umetolewa na Ustadhi Suleiman Habibu ambaye ni mwalimu wa Madrasati Taalimu iliyoko Buhongwa wilayani Nyamagana alipokuwa akitoa nasaha baada ya kimfungisha ndoa mfanyakazi wa Radio Kwizera Majidi Godwin Bruchaed.

Ustadhi Habibu amesema kijana anapofunga ndoa takatifu kwa imani ya dini yake anapata baraka katika familia na kupata watoto kwenye kutambulika kisheria kwa kuwajengea misingi iliyojengwa kutoka kwa wazazi

Amewataka wanadoa kuacha michepuko kwa tamaa za kimwili bali wajielekeze kufanya ibada zilizoainishwa kiimani na kwamba familia zenye ndoa takatifu zimejaa upendo heshima na mahusiano mema kwa jamii inayowazunguka.
"Kila mwanandoa amejenga msingi wa kuaminika katika jamii kwa kuwa na mume au mke aliyepatikana akishuhudiwa na ndugu jamaa wakiwemo marafiki hivyo jitunzeni  kwa kuzingatia malezi ya kiimani mpate baraka za watoto  kutoka kwa Mungu" Amesema ustadhi Habibu

Hafla fupi ya ndoa ya Godwin Bichard au Abdulmajid maarufu G2B imehudhuriwa na baadhi ya watumishi wenzake kutoka Radio Kwizera Ngara,  Viongozi wa Chama cha walimu CWT wilaya ya Ngara na Geita pia ndugu jamaa na marafiki kutoka maeneo mbalimbali ya mikoa ya kanda ya ziwa.Post a Comment

0 Comments