habari


Ufaransa Fainali ya Kombe la Dunia 2018 dhid ya England au Croatia.

Wachezaji wa Ufaransa Pogba (left) and Umtiti (right) .  


Bao la Umtiti linamfanya kuwa mchezaji mdogo kuwahi kufunga katika nusu fainali kombe la dunia(miaka 24 na miezi 7), rekodi ambayo imedumu miaka 60 tangu Just Fountaines kufunga mwaka 1958 akiwa na miaka 24 na miezi 10.

Kipindi cha kwanza katika mechi hii kiliisha kwa sare ya bila kufungana huku kukiwa na piga nikupige katika milango ya timu zote lakini hakuna timu iliyopata bao.

Beki Samuel Umtiti aliifungia Ufaransa bao pekee na la ushindi dakika ya 51 katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Ubelgiji kwenye mchezo wa Nusu Fainali Kombe la Dunia leo July 10,2018 kwenye Uwanja wa Saint-Petersburg nchini Urusi.

Ufaransa itakutana na mshindi wa Nusu Fainali ya pili kesho July 11, 2018  kati ya England na Croatia.

Post a Comment

0 Comments