habari


Tsh Laki 4 za Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji zamponza Mwenyekiti na Kutakiwa Kujiuzulu.

Wananchi wa Kijiji cha Buhororo wilayani Ngara mkoani Kagera wakiwa Mkutanoni.

Shaaban Ndyamukama, Rk Ngara. 

Wananchi wa kijiji cha Buhororo wilaya ya Ngara mkoani Kagera wamemtaka mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Stanford Simon kujiuzuru baada ya kufanya ubadhilifu wa fedha Shilingi 477,000  walizochanga kujenga Zahanati.

Hayo yamebainika jana katika mkutano wa kijiji na kwamba fedha hizo zinahusisha wananchi 46  ambao walimkabidhi fedha walizopata kutoka mpango wa kusaidia kaya maskini TASAF kuchangia zahanati bila kupatiwa stakabadhi na kusababisha ujenzi huo kukwama baada ya kufikia hatua ya msingi.

 
Mwenyekiti wa Kijiji (kushoto) amekiri kutumia Fedha hizo0 anaetuhumiwa kula fedha hizo.

Mwenyekiti wa kamati ya mipango  na fedha wa serikali ya kijiji Emily Simon  amesema fedha hizo zimepotea katika mazingira ya kutatanisha kuitumia bila kukubaliwa na wajumbe wa  serikali ya kijiji hivyo kukiuka miiko ya uongozi na utawala bora

Alisema  wananchi  wa kijiji hicho wapatao 4000 walioko katika kaya 874 kila kaya ilipangiwa kuchangia  Shilingi 30,000 ambapo  michango  inalipwa rejareja  na zahanati ilijengwa msingi  na mafundi walitakiwa kulipwa  Shilingi 4.7 milioni  kwa miezi mitatu.

Alisema mpaka sasa mafundi na vibarua wanaidai serikali ya kijiji Shilingi 1.7 milioni hivyo kusababisha wananchi kukata tamaa ya kuendelea kuchangia baada ya Mwenyekiti wa kijiji kutumia fedha zao bila kupara ridhaa yao.

 
 
Katika michango ya ujenzi wa zahanati zilikusanywa Shilingi 3, 723, 000 lakini  baadhi ya wananchi walilalamikia kutokabidhiwa stakabadhi ya malipo  kutoka kwa Mwenyekiti wa serikali za kijiji  akidai  havikuwepo  vitabu vya halmashauri ya wilaya na kuandikwa majina yao kwenye daftari.

Aidha mmoja wa wakazi wa kijiji hicho Philmon Burchard aliwataka wananchi kupiga kura ya kutokuwa na imani kwa Mwenyekiti wa kijiji na kushinikiza ajiuzulu kwa kuwa hawezi kuhimiza maendeleo na kuwathibiti wahalifu wakati yeye ni mtangulizi wao.

Matukio ya uhalifu ambayo ulikemea mbele yetu na  viongozi wa wilaya katika mikutano na vikao ilikuwa  danganya toto, kwamba wewe ni msimamizi wa kamati ya ulinzi na usalama ondoka na tukulaze rumande” Alisema Buchard maarufu Msoja.

 
 
Akijibu hoja za wananchi hao, Mwenyekiti wa kijiji hicho Sraford Simon alikiri kutumia fedha za ujenzi wa zahanati ambazo zililenga kuwalipa mafundi  na kuomba kuzilipa kwa awamu akiandika barua ya kuthibitisha malipo kwa muda wa miezi mitatu

Alisema alijikopesha kutokana na kuuguliwa na mke wake na kulazimika kumpeleka Hospitali na kwamba atatafuta kila inavyowezekana kulipa fedha hizo hivyo wamvumilie  kwa kuwa amekiri na kudhihirisha kulipa mbele ya wananchi.

Nakiri mbele yenu na kwa maandishi kupitia kamati ya mipango uchumi na fedha, nisingeliacha mke wangu apoteze maisha wakati nilishikilia fedha za kijiji hivyo nilijikopesha na kumpeleka hospitali kwa ajili ya matibabu” Alisema Simon

Wananchi waliomba Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ngara  kutoa vitabu vya stakabadhi kukusanyia michango  ya ujenzi wa miradi ya maendeleo kwani wanadhulumiwa kutokana na kuandikwa majina kwenye karatasi pekee zinazopotezwa.

Post a Comment

0 Comments