habari Mpya


Sherehe ya Miaka 15 tangu kuanzishwa kwa Shule ya Msingi ya Mtakatifu Inyasi Mkoani Dodoma.

Wanafunzi wakionesha Somo la Sayansi kwa Vitendo wakati wa Sherehe ya Miaka 15 ya Kuanzishwa kwa Shule ya Msingi Mtakatifu Inyasi mkoani Dodoma.


Shule hii ya Mtakatifu Inyasi iliyoko Mkoani Dodoma ilianzishwa na Mapadre wajezuiti mwaka 2002 na inaendeshwa kwa kushirikiana na Masista wa Mt. Gemma wa Jimbo la Dodoma.

Ilianzishwa chini ya usimamizi wa Padre Damas Missanga aliyekuwa Paroko na Mkurugenzi wa kwanza wa shule.

Katika Hafla hiyo,Mgeni rasmi alikuwa ni Mhe.Anthon Peter Mavunde ,Mbunge na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu.

Maonesho ya Elimu kwa Vitendo na Nadharia shule ya Awali na Msingi  ya Mtakatifu Inyasi.
Post a Comment

0 Comments