habari Mpya


Serikali ya Tanzania yatoa milioni 400 kuboresha kituo hicho cha Afya Uvinza mkoani Kigoma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Ummy Mwalimu akikagua ujenzi wa moja ya nyumba za watumishi katika Kituo cha Afya Uvinza wilayani Uvinza mkoani Kigoma wakati wa ziara ya kuangalia hali ya utoaji huduma za afya mkoani humo.

Na Adrian Eustaus – RK Kigoma.

 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Ummy Mwalimu amewataka wadau wa maendeleo katika sekta ya afya kuwekeza nguvu katika masuala yanayowagusa wananchi moja kwa moja.

Waziri Ummy ameyasema hayo wakati alipotembelea Kituo cha Afya cha Uvinza kilichopo wilayani Uvinza mkoani Kigoma katika ziara yake ya kujua hali ya utoaji wa huduma za afya mkoani humo.

"Nataka kuona wadau wa maendeleo ya afya wanakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi hususan huduma za afya ya mama na mtoto kuliko kujikita kwwnye semina", alisema Waziri Ummy.
 
Mbali na hayo katika ziara hiyo Waziri Ummy amesema kuwa Serikali ya Rais John Pombe Magufuli kupitia Wizara yake imetoa milioni 400 kuboresha kituo hicho cha Afya Uvinza mkoani Kigoma lengo likiwa ni kuimarisha huduma za afya kwa Wananchi.

Aidha Waziri Ummy amewataka viongozi wilayani Uvinza kusimamia vema matumizi ya fedha hizo pamoja na kuhakikisha ujenzi huo unamalizika kwa wakati.

Kukamilika kwa Ujenzi wa kituo hicho,Wananchi wataweza kupata huduma za Upasuaji, Ex-ray, Kulaza Wagonjwa, Dawa aina zote, Ultra Sound nk.
 

Post a Comment

0 Comments