habari Mpya


Serikali kuimarisha Ushirika ili Wakulima Wanufaike na Kilimo Chao.

Mkulima Odas Mathayo na matarajio yake ni kuvuna kahawa aina ya robosta kilo 400 baada ya kupanda miche 300  ndani ya shamba lenye ukubwa wa ekari moja tangu alianzishie kilimo cha kahawa mwaka 2010 katika kijijini Buhororo wilayani Ngara mkoani Kagera-Picha na Maktaba Yetu.

 Na Anord Kailembo –Rk Bukoba.

Wizara ya Kilimo imesema itahakikisha inaimarisha ushirika nchini ili kuwawezesha wakulima wa mazao mbalimbali wananufaika na kilimo chao.

Naibu Waziri wa Kilimo Bw. Omary Mugumba amesema hayo wakati akizungumza na viongozi, Wataalam na Wadau wa Kilimo cha zao la Kahawa mkoani Kagera wakati wa ziara yake aliyoifanya hii July 4, 2018 kwa lengo la kujionea hali ya uzalishaji wa Kahawa na changamoto zake.

Ni Naibu Waziri wa Kilimo Bw,Omary Mugumba akisalimiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Kagera wakati wa ziara yake mkoani humo ya kujionea changamoto zinazolikabili zao la Kahawa.

Amesema kuwa ili mkulima aweze kunufaika na kilimo ni lazima ushirika unao msimamia uwe imara kuanzia kwenye mfumo uliowekwa wa usimamizi na ushirikiano mzuri na wakulima.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kagera ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Bukoba Bw. Deodatus Kinawilo amesema kuwa tayari vyama vya ushirika vinasimamiwa ili vitekeleze vyema maagizo yanayotolewa na serikali katika kuhakikisha mazao ya kimakakati yanayolimwa mkoani Kagera yanamnufaisha mkulima.

Post a Comment

0 Comments