habari Mpya


RC Kigoma-''Aagiza Miradi ya Maji ikamilike kwa Wakati Kibondo na Kakonko.

Moja ya masuala makubwa yanayoathiri Watanzania wengi wanaoishi Vijijini ni uhaba wa Maji Safi.
 Pichani ni Kijana akichota Maji –Picha kwa Hisani ya ASCFKibondo.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga amewaagiza Wakuu wa wilaya za Kibondo na Kakonko pamoja na Wahandisi wao kusimamia Miradi ya Maji  ikiwemo Mradi wa Maji Muhange wilayani Kakonko uweze kutoa maji kwa wananchi kabla ya mwezi huu kukamilika.

Kauli hiyo ameitoa akiwa katika ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya Miradi ya Maji ndani ya wilaya ya Kakonko ambapo amesikitishwa kukuta mradi wa maji Muhange haujakamilika licha ya kwamba ulianza kutekelezwa tangu mwaka 2012 kwa ufadhili wa benki ya dunia.

Brigedia Jenerali Mstaafu Maganga amesema ni jambo la kushangaza kuona Wananchi wanaendelea kupata shida ya maji huku mradi ukiwa umefungwa kwa changamoto ndogo ndogo ambazo zinaweza kufanyiwa marekebisho.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagalla akipokea maelekezo hayo, ameahidi kwenda kukaa pamoja na Viongozi hao kujadiliana ili kuweza kukamilisha lengo la Serikali kufadhili miradi ya maji kwa wananchi.

Post a Comment

0 Comments