habari Mpya


Padre Wilson Kasigwa:Waumini tuwaheshim viongozi kwani wanamchango mkubwa katika jamii

MULEBA:SHAFIRU YUSUFU
Wakristo wilayani Muleba Mkoani Kagera wametakiwa kuwaheshinu viongozi wao na kuwaona kuwa wana mchango mkubwa katika jamii.

Hayo yamebainishwa na mwalimu mlezi wa seminari ya Rubya Padre Wilson Kasigwa kutoka Jimbo katoliki la Bukoba kwenye misa ya shukurani ya Padre mpya Revokatus Mwemezi iliyofanyika leo katika kijiji cha Karambi parokia ya Ngote wilayani Muleba.

Padre Kasigwa amesema kuwa viongozi hao wamekuwa wakidharauliwa wakati ni wahudumu wa kiroho katika jamii na kimwili ili kulinda maadili kwenye Maeneo waliyopo.
“Niwaombe sana wapendwa katika kristo tuwaheshim sana viongozi wetu kwani wanamchango mkubwa sana katika jamii ilikuendelea kuwa nakizazi kinacho mtii Mungu kwakufanya yale yanayo mpendeza mwenyezi Mungu na muumba wetu”alisema Padre Kasigwa

Kwa upande wao baadhi ya waumini waliokuwa kwenye misa hiyo wamesema ili kuondoa hali ya viongozi kutoheshimiwa ni wajibu wa wazazi na walezi kushirikiana ili kuweka hali ya upendo.


Padre Revocatus Mwemezi amepadrishwa June 30 mwaka huu na askofu wa Jimbo katoliki la Bukoba muhashamu Desderius Rwoma katika parokia ya ya Ngote na atafanya utume katika Jimbo hilo.
Post a Comment

0 Comments