habari Mpya


Nusu Fainali Kombe la Dunia-Ubelgiji na Ufaransa Julai 10,2018.

Ubelgiji imewashangza wadau wengi wa soka baada ya kutinga nusu fanali ya michuano ya Kombe la Dunia 2018 kwa kuiondosha Brazil kwa kuifunga mabao 2-1.

Kevin De Bruyne alikuwa shujaa baada ya kuifungia bao la pili kwa Ubelgiji dakika ya 31 katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Brazil Jana July 6, 2018 Uwanja wa Kazan Arena nchini Urusi kwenye mchezo wa Robo Fainali Kombe la Dunia. 

 
 
Bao la kwanza la Ubelgiji lilifungwa na Fernandinho dakika ya 13, wakati la Brazil lilifungwa na Renato Augusto dakika ya 76 na sasa watakutana na Ufaransa katika Nusu Fainali Julai 10,2018 kwenye Uwanja wa St Petersburg.

 
 
Ufaransa walishinda bao 2-0 dhidi ya Uruguay kwenye mchezo wa robo fainali ya  mapema kwenye Uwanja wa Nizhny Novgorod.

 Ubelgiji sasa itapambana na Ufaransa Julai 10 katika mchezo wa nusu fainali na mara ya mwisho timu hizo zilikutana mwaka 2015 katika mchezo wa kiraļ¬ ki ambapo Ubelgiji ilishinda mabao 4-3. 

Mafanikio ya mwisho kwa Ufaransa kwenye Kombe la Dunia ni kumaliza nafasi ya pili mwaka 2006 na Ubelgiji ni kutinga hatua ya robo fainali mwaka 2014.

 

Post a Comment

0 Comments