habari Mpya


Mwandishi wa Habari na matangazaji wa Radio kwizera Maria Philiberth Atwaa tuzo ya mwandishi mahili wa habari za Utapiamlo.

Maria Philberth ambaye ni mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio kwizera ameshinda tuzo ya Mwandishi mahili wa habari za Utapiamlo.

Katika tuzo hizo amekuwa mshindi wa kwanza na mshindi wa Jumla hapa nchini Tanzania kwa kuwashinda wandishi wenzake waliokuwa wakishindananaye kuwania tuzo hizo.

Tuzo hizo zilizo tolewa na shirika la {CIP} International Potato  Centre 2018,Mgeni rasmi alikuwa waziri wa kilimo Charles Tizeba ambaye amemkabidhi tuzo hizo Maria.
Akizungumza na Radio kwizera fm kupitia kipindi cha Mseto leo Maria amesema siri ya mafanikio ni kujituma ndichokilicho mfikisha hapo katika mafanikio hayo.

“Namshukuru Mungu leo nimepata tuzo napenda kuishukuru timu nzima ya Radio kwizera kwaushindi huu nilio upata akiwemo Auleria Gabriel na mwalimu Noel Tomson kutoka BBC Media Action kwa ushirikiano wao walio nipatia bila kuwa sahau viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Ngara na mkoa Kagera Kwaujumla mpaka kufanikisha kipindhi hiki ambacho kime nipatia tuzo hii leo”Amesema Maria  


Post a Comment

0 Comments