habari Mpya


Muhasibu wa Radio kwizera Deusdedith Byebarilo Aondokewa na Mama mzazi

BUKOBA  NA SHAABAN NDYAMUKAMA RK
Jamii iliyo  katika madhehebu mbalimbali ya kidini imeshauriwa kujenga tabia na mazoea ya kuwaombea marehemu ambao ni wazazi ndugu jamaa na marafiki  huku wakiwaenzi kwa matendo mema baada ya kutimiza siku za kuishi duniani.


Hayo yamebainishwa na Paroko wa Parokia ya Kasherero jimbo katoliki la Bukoba Mkoani Kagera Padre Henery Kempanju wakati wa mahubiri katika  ibada ya misa ya mazishi ya mama mzazi wa Brother Deusdedith Byebarilo ambaye ni Mhasibu wa Radio Kwizera iliyofanyika leo Kijijini kwao Burugo kata ya Nyakato wilaya ya Bukoba viijini
Padre Kempanju amesema katika kuwaombea marehemu wafanye mawasiliano na viongozi wao wa kiimani kuwaelekeza la kufanya na misa ya kuwaombea hailipiwi fedha yoyote ispokuwa kwa kuwa ni wajibu wa kiongozi husika kutekeleza wajibu wake

Aidha amewataka waazi kutimiza wajibu wao wa kuwalea watoto wao kimaadili kwa kuwapatia mambo matatu ambayo ni chakula matibabu na kemeo lisiloumiza badala ya kuwachia wafanyakazi katika  taasisi za elimu wakiwa katika umri mdogo.

Katika hatua nyingine amewahimiza wanandoa katika familia kuwa na moyo wa kuhurumiana wakioneshana upendo ambapo wanaume wajihadhari na vitendo vya kuwapiga wake zao kwa mateke mithili ya anayewasha pikipiki na kwamba vitendo vya uongo, uchonganishi,umbea havitahili hats mbele za Mungu.

"Baadhi yetu kutoka kanisa katoliki tunakuwa na umbea kwa maaskofu juu ya matendo ya mapadre, watawa, na hata wanafamilia wakituhumianana kwa uasherati au uzinzi janani sote ni binadamu hakuna mkamilifu"Amesema Padre Kempanju.
Mahubiri ya Paroko huyo kwenye msiba yamewaondolea simamzi na huzuni  ghafla kwa kucheka kufurahia alichowahusia kutokana na kuchanganya lugha ya kiswahili na kihaya huku akitafrisi kwa wasiofahamu lugha hizo.

"Msichana alipopata mimba kwa uasherati alifukuzwa ili aweze kirejea kwao alitozwa faini ya mbuzi na kukaa nyumbani sio kama hivi sasa mambo ya kidijitali ingawa sijaruhusu uasherati na uzinzi viendelee kufanyika la hasha" Amesema
Mama yake Brother Deus Byebariro aliyeitwa Imelda Byebariro Rugomora amefariki akiwa na umri wa miaka 76 akiacha watoto wanane kati ya 11 aliojaliwa kuwazaa  ambapo wajukuu ni 28 na vitukuu watatu akitokea familia ya Chifu Rugomola wa Maruku mkoani Kagera 
Mazishi yake yaliongozwa na Padre huyo Kempanju ,Padre Damas Missanga, kutoka Radio Kwizera Ngara na padre Pascal Mwijage chini ya kwaya ya kikatoliki kutoka kigango cha Kahororo na waumini wa madhehebu mbalimbali ya kidini kutoka maeneo mbalimbali vikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama
Pichani ni sehem ya watu walio hudhuria katika idaaba ya Mazishi.


Pichani wa kwanza kushoto ni Brother Deusdedith  Byebarilo Muhasibu wa Radio kwizera aliye fiwa na Mama yake Mzazi na pembeni yake ni Afisa masoko wa Radio kwizera Donatus Bartazari wakiteta jambo

Pichani ni Baadhi ya Wafanyakazi wa Radio kwizera walio fika kumfariji Br.Deus
Brother Deusdedith ni Bruda kutoka 
shirika  la watawa wanaume wa katoliki wa marafiki wa Yesu    {Jesuit Fathers}.

Post a Comment

0 Comments