Source; RK, SY (afya)
Ed: FM
Date: Monday, July 30, 2018
MULEBA
Serikali imetenga Jumla
ya shilingi bilioni 30 kwa ajili ya kuboresha
hospitali za Rufaa za
mikoa kwa mwaka wa fedha wa 2018 na 2019
Naibu waziri wa Afya,
maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto Dr Faustine Ndugulile amesema hayo
akizungumza na waganga wakuu wa wilaya Mkoani Kagera
Aidha amewataka watoa
huduma ya afya walioko kwenye vituo vya afya na
zahanati kila mwanzo wa
wiki wawe wanaorodhesha dawa zilizopo kwenye
vituo vyao ili kuondoa
usumbufu kwa wananchi
Insert….naibu
waziri wa afya
Cue in….
Cue out…
Awali akisoma taarifa
mganga mkuu wa Mkoa wa Kagera Dkt Marco
Mbata amesema kuanzia January hadi June mwaka huu vifo vya wakina mama ni
41 ambapo vifo vya watoto vimefikia 368 kutokana na ukosefu wa damu
Source; RK, SD (huduma)
Ed: FM
Date: Monday, July 30, 2018
KAHAMA
Wakazi wa kijiji cha
Nshiba kata ya Chona halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga
wanakabiliwa na tatizo la uhaba wa maji hasa katika kipindi hiki cha
kiangazi baada ya visima vitatu kati ya
sita walivyovitegemea kukauka
Kauli hiyo imetolewa na
wakazi hao kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na Mbunge
wa jimbo hilo ambaye pia ni Naibu waziri wa ujenzi Bw Eliasi
Kwandikwa ambaye alifika kwenye kijiji hicho kwa ajili ya kusikiliza kero
za wananchi
Wamesema wanaamka usiku
wa manane kwenda kutafuta maji jambo linalohatarisha maisha yao na kwamba
wanaiomba serikali kuwatafutia ufumbuzi wa suala hilo
Insert….Lucy
Cue …in
Cue …out
Kwa upande wake mbunge wa
jimbo la Ushetu Bw Eliasi Kwandikwa amewaambia wananchi kuwa
serikali imetoa zaidi ya shilingi milioni 600 kwa ajili ya kutengeneza mradi
mkubwa wa maji katika kata ya Chona jambo ambalo litasaidia kuondoa kero ya
maji kijijini humo
Source; RK, SM (kujiua)
Ed: FM
Date: Monday, July 30, 2018
KIBONDO
Mwanaume mwenye umri wa miaka 50 mkazi wa kijiji cha Nyarugusu kata ya
Kizazi Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma amefikishwa kwenye ofsi ya Afisa mtendaji
wa kijiji hicho baada ya kutaka kujiua kwa kutumia kisu
Akiongea na redio kwizera afisa mtendaji wa kijiji cha Nyarugusu Bw
Shedrack Totoye amesema tukio hilo limetokea usiku wa July 29 mwaka huu
katika kitongoji cha Bugwana baada ya mwanaume huyo kufika nyumbani kwake akiwa
amekunywa pombe
Amesema baada ya mwanaume huyo kupelekwa ndani na mke wake ndipo alipata
hasira kwa madai kuwa wamefanya makosa kumtoa mahali alipokuwa amelala nje
ya nyumba yake
Insert……Bw Totoye
Que in…………
Que out……….
Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha Bugwana Bw Castory
Ntaburanyina amesema kitendo ambacho alitaka kukifanya Bw Churila ni cha kwaza
kutokea kwenye familia hiyo na kwamba ni vyema jamii zikajijengea utamaduni wa
kufika kwenye ofsi za viongozi kuliko kuchukua maamuzi magumu ya kujiua
Source; RK, AE (uzalishaji)
Ed: FM
Date: Monday, July 30, 2018
KIGOMA
Zaidi ya hekta ishirini
na tatu zinazomilikiwa na shirika la hifadhi ya jamii NSSF katika eneo la
Nyabigina Wilayani Kigoma Mkoani Kigoma zinatarajia kutumika katika uzalishaji
wa bidhaa mbalimbali ikiwemo mafuta ya Mawese yanayolimwa kwa wingi na wakulima
wa mkoa huo
Akitoa taarifa juu ya
eneo hilo afisa mtendaji wa kata ya Mwandiga Bw Frank Mandali amesema wapo
baadhi ya wananchi wanaodai fidia baada ya viwanja vyao kujumuishwa katika eneo
hilo na hivyo shirika kutakiwa kulipa fidia kabla ya kuanza shughuli za
uzalishaji
Insert…………………..Frank
Que in……………kuna watu
Que out…………kudai
Akitoa ufafanuzi wa suala
hilo meneja wa NSSF mkoani Kigoma Bw Saidi Tandika amesema ipo mikakati
inayoendelea kwa ajili ya kumaliza changamoto hiyo na kwamba miongoni mwa fidia
zitakazo tolewa ni pamoja na nyumba na mashamba
Kwa upande wake waziri wa
ajira kazi na vijana nchini Bi Jenista Mhagama amesema kwakua eneo hilo lipo
mkabala na mashamba ya michikichi linatakiwa kutumika katika uzalishaji wa
mafuta aina ya mawese yatakayosaidia kuinua uchumi wa wakulima
Insert………….Jenista
Que
in…………ukiliangalia
Que
out……yakafanyika
Source; RK, LT (Ulinzi wa
watoto)
Ed: FM
Date: Monday, July 30, 2018
KINSHASA
Wazazi na walezi katika mji wa Kindu mkoa wa Maniema
mashariki mwa DRC wameshauriwa kulinda vyema watoto wao na kuepuka kuwatumia
kama sehemu ya biashara zao
Shauri hilo limetolewa na mwanasheria Michel Masumbuko katika
mazungumzo na waandishi habari ambapo amesema wakati huu ambapo shule
zimefungwa watoto wanatumia muda wao mwingi kuuza biashara hali inayohatarisha
usalama wao
Amesema mtoto anahitaji kupumzika huku akiiomba serikali
kutoa ajira kwa wazazi na kuzidisha mishahara kwa wafanyakazi
Insert… Michel Masumbuko
Cue In:
Cue Out:
Nao baadhi ya washiriki kwenye mkutano huo wamesema umaskini
na ukosefu wa ajira ni chanzo kikubwa kinacho pelekea wazazi kutumia watoto
katika kutafuta riziki ya familia na kuwfanya watoto kujitafutia riziki zao
wenyewe bila kutegemea wazazi
|
0 Comments