habari Mpya


Mbappe atwaa tuzo ya mchezaji bora Chipukizi Kombe la Dunia 2018 huku Luca Modric akitwa tuzo ya mchezaji bora.

Kiungo wa Ufaransa na Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe, ametangazwa kuwa ndiye mshindi wa tuzo ya mchezaji bora chipukizi katika fainali Kombe la Dunia 2018 iliyofanyika jana.
Licha ya kuvunja rekodi nne kwenye michuano hii, ikiwa ni pamoja tuzo ya mchezaji mwenye umri mdogo kuwahi kucheza kombe la dunia, rekodi ya kinda aliyewahi kufunga mabao mawili kwenye Kombe la Dunia, rekodi ya kinda aliyefunga kwenye mechi ya fainali na rekodi ya kutwaa kombe, Mbappe ndiye mchezaji bora wa mashindano haya.


Mbappe amekuwa mchezaji wa pili wa Ufaransa kuwahi kushinda tuzo hiyo, baada ya Paul Pogba aliyeshinda tuzo hiyo miaka minne iliyopita. Tuzo hiyo inaweza ikashindwa na mchezaji aliyezaliwa na baada ya Januari mosi.


Kigezo kingine kinachotumiwa kupata mshindi wa tuzo hiyo ni ufundi uwanjani, kasi, utundu udambwidambwi, mchango kikosini na uungwana mchezoni, kwa mujibu wa kamati ya ufundi ya FIFA. 


Mbappe amefunga mabao manne kwenye michuano hii, ikiwemo bao la nne, katika ushindi walioupata kwenye fainali dhidi ya Croatia.


Wakati huo huo Kiungo  na Nahodha wa Timu ya Taifa ya Croatia, Luka Modric ameibuka mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 na kupewa Mpira wa Dhahabu wakati timu yake ikipoteza mchezo wao wa fainali kwa kukubali kichapo cha bao 4-2 kutoka kwa Ufaransa huko Urusi.

Modric ambaye amemaliza mashindano akiwa na mabao mawili, ameisaidia timu yake kutinga fainali ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu hiyo kufikia hatua hiyio kubwa ya kihistoria.

Modric amewashukuru mashabiki wa Croatia na wachezaji wenzake kwa sapoti kubwa waliowapa hadi kufikia fainali licha ya kufungwa.

Mbelgiji, Eden Hazard amekuwa mchezaji Bora wa Pili na kutunukiwa mpira wa Silver, na Mfaransa, Antoine Griezmann ameibuka mchezaji Bora wa Tatu na kupewa mpira wa shaba.

Wachezaji wengine ambao wamewahi kubeba tuzo hiyo ni pamoja na Lionel Messi, Zinedine Zidane, Ronaldo de Lima, Davor Suker, Diego Maradona na Paolo Rossi.
Tuzo hii, inamuweka Modric katika nafasi nzuri ya kushinda tuzo ya mwaka huu ya Ballon d'Or.

Post a Comment

0 Comments